Tangazo

October 29, 2013

Mbunge wa Temeke Mtemvu na Diwani wa Kurasini Kimati wapiga Stop malori kumwaga maji taka katika mabwawa ya Kurasini

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu  akimuuliza swali Mfanyakazi wa  Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASA),Omar Mlanzi, walipokwenda kupiga marufuku malori kwenda kumwaga maji taka katika mabwawa ya Kurasini, Dar es Salaam, baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kulazwa hospitali kwa kuhara na kutapika kulikosababishwa na Dawasa kutoweka dawa ya kuua bakteria kwenye mabwawa hayo.Sababu nyingine ni kwamba mabwawa hayo yamezidiwa baada ya mabwawa mengine jijini kufungwa hivyo malori yote ya taka kwenda kumwaga hapo. Wa pili ni Diwani wa Kata hiyo, Wilfred Kimath na Augustino ambaye ni mtumishi wa kampuni binafsi iliyopewa jukumu la kusimamia malori yanayokmwaga mati taka katika mabwawa hayo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtemvu akijadiliana jambo na Diwani, Kimath.
 Baadhi ya malori yaliyokutwa yakimwaga maji taka kwenye mabwawa hayo.
 Moja ya malori lililokutwa likimwaga maji taka kabla ya kupigwa marufuku.

 Mtemvu akiwasiliana na uongozi wa Dawasco na Dawasa.
 Moja ya mabwawa likiwa limefurika maji taka kupita kiasi.
 Mfanyakazi wa lori akifunga baada ya kuamriwa kufanya hivyo.
 Mmoja wa madereva  Hemed Abdalah akielezea adha wanayipata baada ya mabwawa ya maji taka kufungwa jijini.
 Mtemvu kulia akiangalia baadhi ya malori ya maji taka.
Mtemvu na Kimath wakiondoka baada ya kufunga matumizi ya mabwawa hayo.

No comments: