Tangazo

October 29, 2013

WASANII WAASWA KUTUMIA FURSA YA MFUKO WA VIJANA

 NA MAGRETH KINABO - MAELEZO

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (pichani), amewataka wasanii nchini kutumia Mfuko wa Maendeleo ya  Vijana kwa ajili ya kukopa fedha za kuendeleza kazi zao .

 Profesa   Gabriel  alisema hayo jana wakati alipokutana na  baadhi  viongozi wa mashikisho  ya wasanii na wasanii kwa nyakati tofauti jijini  Dares Salaam kwenye ukumbi wa wizara  hiyo.

 Alisema Serikali imetenga fedha  kiasi cha Sh. bilioni 6.1 kupitia mfuko huo, ambapo kati ya fedha hizo Sh. bilioni 1.4 za makundi maalum wakiwemo wasanii.  Hivyo  ni vyema  wasanii vijana wakaanza kutumia  fursa hiyo.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu huyo   aliwataka wasanii   kuzingatia maadili na kujenga heshima katika  utendaji wa kazi zao michango ya iendelea kutambulika kwenye jamii.

 Profesa Gabriel aliyasema  hayo jana  wakati alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kuhusu Haki miliki kwa wasanii  iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga jijini   Dares Salaam.

 Alitoa wito kwa wasanii   hao kuacha kusema kwani tabia hiyo inaharibu majina yao kwa kuwa itakuwa ni vigumu jamii kuthamini  michango yao iwapo watajihusisha na vitendo viovu, huku akisisitza kwamba wasanii ambao  majina yao yameshajengeka  katika jamii watambue kuwa huo ni mtaji wao wasiupoteze.

 Aliwataka kuanza kufanya kazi zao  kibiashara  na kuwa taaluma ya biashara ili waweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi, ikiwemo kutumia mapato ya kazi zao katika kufanya shughuli zingine.

 Alisema  Serikali itaendelea kushirikiana na wasanii katika kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazozikabili.

Kwa upande wake msanii maarufu  John Kitime akizungumza kwa niaba ya wenzake alivitaka vyombo vya habari viwe vinalipia  kazi zao wasanii pale wanapotumia nyimbo zao.

 Naye mmoja wa kiongozi, Rais  Shirikisho la Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF), Simon Mwakifamba aliomba wapewe nguvu ya kisheria ili kuweza kudhibiti maadili ya wasanii kauli ambayo ilingwa mkono na baadhi ya viongozi   wenzake.

Kwa upande wao wasanii hao , waliiomba Serikali kutawasaidia kutatua tatizo la uharamia wa kazi za wasanii,ambapo Suzan Lewis   alishauri kuwa ikiwezekana utumika mfuko unatumika kwenye vocha za simu ambazo mtu hawezi kughushi.
 Pia walipendekeza kuwepo kwa bei elekezi  ili kudhibiti uuzaji holela kwa kazi zao.

No comments: