Meneja wa Huduma za Jamii
wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kushoto) akizungumza kwenye simu
na mmoja wa washindi wa droo ya wiki ya promosheni ya Mimi Bingwa.
Kulia ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Mchezo wa Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh.Picha
na Mpiga Picha wetu
########################################
Dar es Salaam. Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania, imezawadia wateja wake zaidi ya Sh130 milioni na tiketi 12 za safari
iliyolipiwa kila kitu kwenda Old Trafford, nchini Uingereza.
Promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyoanza mwishoni mwa Novemba
mwaka jana, inalenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa jamii
inayoizunguka. imeshuhudia wateja 82 wakiibuka washindi katika droo za kila
siku na kila wiki.
Akizungumza baada ya kupata washindi wa wiki ya kwanza ya awamu
ya pili juzi, Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayuni alisema
zaidi ya Sh324 zilitengwa kama zawadi ya fedha taslimu kwa ajili ya promosheni
na mwenendo wa idadi ya pointi za washiriki unazidi kutia hamasa.
“Mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea kujikusanyia
alama unazidi kuvutia. Watu wengi wameona wakicheza zaidi wanajikusanyia alama
Zaidi, hivyo kujiongezea nafasi zao za ushindi bado kuna zawadi nyingi, ikiwamo
zawadi kubwa ya Sh50 milioni,” alisema Bayuni.
Mmoja wa washindi wa droo ya wiki hii, Saidi Kitambuliyo,
alishukuru Airtel kwa kumsaidia kuanza mwaka kwa kishindo. “Fedha hizi zimekuja
wakati mwafaka… bahati nasibu iliyoruhusiwa na Serikali ni sawa na uwekezaji,”
alisema.
Pia, Bayuni alisema washindi wa tiketi watapata fursa ya kuchagua
mtu mmoja atakayeongozana naye kufurahia safari hiyo.
No comments:
Post a Comment