Tangazo

January 16, 2014

Wawili wazoa Milioni 10/- za Airtel

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando
Da es Salaam. Mkazi wa Songea mkoani Ruvuma, Rehema Mohamed Nasibu na Willhard Mlenga Malimbo wa jijini Dar es Salaam wametwaa kitita cha Sh5 milioni kila mmoja katika promosheni ya Mimi Bingwa inayoendeshwa na Kampuni ya Simu ya Airtel, inayoendelea.

Washindi hao walitangazwa juzi na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando wakati wa kuwatangaza washindi mbalimbali wa droo ya wiki ya nane ya promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Mbali na washindi hao, washindi wengine 10 walijishindia Sh1 mil kila mmoja. “Tumeona wateja 108 wakiibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki.”

“Mpaka sasa, Airtel imeshatoa zawadi ya zaidi ya Sh170 mil kwa washiriki wa promosheni hiyo iliyoanza Novemba mwaka jana,” alisema Mmbando.

Katika droo ya kila wiki iliyochezeshwa juzi, Michael Shiri (Dar), alishinda tiketi mbili za safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda England kuangalia moja ya mechi za Man United.

No comments: