Tangazo

March 22, 2014

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YATOA TAARIFA



 Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam kuhusiana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Pamoja nae ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima. 
 *********
 1.0     UTANGULIZI

 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu makuu mawili; kwanza ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa ajili ya masomo ya Shahada au Stashahada ya juu. 
Jukumu la pili ni kukusanya marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994.

2.0        UTOAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
 Tangu kuanzishwa kwake, Bodi imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa. Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa mikopo kwa Wanafunzi 42,729 wa elimu ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni 56.1.

Idadi ya Wanafunzi wa elimu ya juu wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka kutoka  wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi Wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013. Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4% kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.

Kwa mwaka wa masomo 2013/2014, jumla ya wanafunzi 95,178 wamenufaika na mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi cha TZS 223,977,042,853.00 imekwishalipwa.



Mwaka
Idadi ya Wanafunzi Waliokopeshwa
Ongezeko
(%)
Kiasi kilichoko-peshwa
(Tshs Bilioni)
Ongezeko
(%)
2004/05 (Na Wizara)

16,345

-

9.9

-
2005/2006
42,729
161.4
56.1
467
2006/2007
47,554
11.3
76.1
35.7
2007/2008 
55,687
17.1
110.8
45.6
2008/2009
58,798
5.6
139.0

25.5
2009/2010
72,035
18.4
237.8
28.7
2010/2011
92,791
28.8
230.0
24.5
2011/2012
94,533
2.0
311
35.0
2012/2013
97,348
2.9
335.2
7.2

No comments: