Tangazo

March 22, 2014

MABIBO SECONDARY NA UBALOZI WA JAPAN WASAINI MKATABA WA WENYE THAMANI YA USD 118,873 KWA AJILI YA MRADI UJULIKANAO KAMA "Grassroot Human Security"


Mstahiki Meya wa kinondoni Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa usainishwaji mkataba baina ya shule ya sekondari mabibo na ubalozi wa Japan
 Mstahiki meya akiendelea kuzungumza wakati wa usainishwaji mkataba baina ya shule ya sekondari mabibo na ubalozi wa Japan
 Baadhi ya walimu na wanafunzi wa mabibo sekondari
 Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada akitia sahihi mikataba hiyo
 Mkurugenzi wa Manispaa Eng Mussa Natty wa kwanza kulia akishuhudia utiaji sahihi wa mikataba hiyo
 Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuph Mwenda akiwa na  Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada
 Muonekano wa shule ya sekondari Mabibo
 Majengo ya shule ya sekondari mabibo
Mwalimu alipokuwa anakaribisha Ugeni Kutoka kushoto Mstahiki meya, Balozi wa Japan, Mkurugenz wa manispaa na Mkuu wa Shule ya  mabibo sekondari
mkurugenzi wa manispaa Eng mussa Natty akisalimiana na Mwalimu alipotembele moja ya madarasa kuona ufundishaji unavyoendelea.
Wanafunzi wakifurahia ugeni uliowatembelea  katika shule yao.

 Picha ya pamoja na  Balozi wa Japan na Viongozi wa Manispaa ya kinondoni na Walimu wa mabibo sekondari.
 Balozi akiwa anaondoka eneo la shule ya sekondari Mabibo


Shule ya Sekondary Mabibo iliyopo katika Manispaa ya Kinondoni leo imesaini Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa Maabara ya Kisasa mradi huo unaojulika kwa jina la "Grassroot Human Security" ambao utagharimu kiasi cha USD 118,873 ambazo ni takribani mil 193 za kitanzania umesainiwa leo na Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada mbele ya Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni ndugu Yusuph Mwenda na Mkurugenzi wa Manispaa Eng Mussa Natty. 

Kwa pamoja Wameshukuru sana Serikali ya Japani kwa Msaada huo na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Nchi hiyo na Kuhimiza watoto wapende masomo ya sayansi na kuifanya Kinondoni iwe juu kwa upande Mwingine Balozi Masaki amewataka watanzania kuwekeza Kwenye sayansi na teknolojia kuliko kutegemea kununua kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini vile vile amewashukuru Bi Bernadetha Thomas na Omath Sanga Afisa elimu wa Manispaa kwa kuibua mradi huo.

No comments: