TCRA yazungumzia faida za Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu (Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS)
Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu
faida za Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato
yatokanayo na Simu unaojulikana kama Telecommunication Traffic Monitoring
System (TTMS). Mtambo huo unaweza kutambua mawasiliano ya udanganyifu katika
mitandao na namba za ulaghai zinazotumika kwenye mawasiliano ya kimataifa
kinyume cha sheria. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank
Mvungi.
Naibu Mkurugenzi anayehusika na usimamizi wa Mtambo Maalum
wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato ya Simu (TTMS) kutoka TCRA,
Mhandisi Sunday Richard akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jinsi mtambo
huo unavyofanya kazi ya kudhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za
kimataifa zinazoingia hapa nchini.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-
MAELEZO
No comments:
Post a Comment