Na Magreth Kinabo- Maelezo Dodoma
Wajumbe wengi wa Bunge Maalum la Katiba wamependekeza
kuwepo kwa Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye mfumo wa Serikali mbili, wakati wa kuchambua sura ya
kwanza na ya sita zilizoko katika Rasimu
ya Katiba mpya.
Hayo
yamesemwa leo na wenyeviti wa Kamati namba 10 na moja wa Bunge hilo wakati
wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa St.Gasper mjini Dodoma kwa
nyakati tofauti.
Akizungumzia kuhusu mambo yaliyojiri , Mwenyekiti
wa Kamati namba 10 wa Bunge hilo, Anna
Abdalaah alisema kazi ya kuchambua Rasimu
ya Katiba mpya ainaendelea vizuri na wajumbe wengi wamependekeza mfumo huo huku
wakiwa na sababu zao ambazo zitaoneshwa katika ripoti yao.
Alisema Kamati
yake ina wajumbe 52, ambapo upande wa
Tanzania Bara una wajumbe 37 na Zanzibar 15.
“Hatuna matatizo
ya kutoelewana , kazi inaenda vizuri leo tumemaliza masuala ya shirikisho na muungano
,tumepiga kura hilo halitusumbui, hivi sasa tuko kwenye masuala ya ardhi ,”
alisema Mama Anna.
Aliongeza
kuwa katika kupitia vipengele vya rasimu hiyo yapo mambo ambayo wote
wamekubaliana nayo mfano eneo lote la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote
la Tanganyika likijumuishasehemu yake ya
bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari , ambapo wameongeza mito ,
maziwa, milima na anga.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge hilo, Ummy Ali Mwalimu alisema
katika suala la muundo wa Serikali wengi walitaka suala la Serikali Shirikishi
liondolewe, huku wengi wakisema Ibara
ibaki kama ilivyo.
Ummy aliongeza kuwa wanaendelea na mjadala hadi saa
2:00 usiku, hivyo kesho watapiga kura ili kuweza kumalizia vipengele vingine,
hivyo Ijumaa hawataweza kuwasilisha ripoti yao na ameshamwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, kuhusu suala hilo.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,alisema bila kutaja upande upi alisema
ukigawa upande mmojakatika 2/3 unapata 12 na mwingine saba, ambapo
ikiongeza mtu mmoja unapata 2/3
Naye Mwenyekiti wa Kamati namba moja Profesa Makame Mbarawa, Anna
Kilango Malecela, ambaye Kamati yake ina wajumbe 53, Tanzania Bara 35 na
Zanzibar 18 akizungumza kwa njia ya simu
kwa waandishi wa habari,alisema wajumbe wote wanataka muungano, hivyo hakuna
aliyesema hataki muungano.
Aidha Kilango alisema wapo baadhi ya wajumbe
walitaka serikali mbili na wengine tatu, hivyo wamepisha kuhusu muundo wa
Serikali uweje, hivyo wataendelea kupiga kura jioni.
No comments:
Post a Comment