Sehemu ya wanahabari na wanachama wa MCT waliohudhuria kongamano hilo. |
Mwanachama wa MCT, Simon Mkina akigawa karatasi za kupigia kura katikauchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais na Wajumbe wa Bodi ya MCT, wakati wa mkutano mkuu wa 17 wa wanachama. |
Upigaji wa Kura ukiendelea. |
XXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na John Badi
Daily Mitikasi Blog
Bagamoyo
MKUTANO Mkuu wa 17 wa Wanachama wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), umemchagua Jaji mstaafu Thomas Bashite Mihayo kuwa Rais mpya wa baraza
hilo, baada ya aliyekuwa Rais Jaji mstaafu Dk. Robert Kisanga kumaliza muda
wake.
Mkutano huo, ulioenda sambamba na Kongamano la Mwaka la
Maadili ya Waandishi wa habari ulifanyika katika eneo yatakapo kuwa makao makuu
ya baraza hilo, Kimalang’ombe wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani juni 24 na 25
mwaka huu.
Aidha katika uchaguzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Zanzibar (ZBC), Hassan Abdallah Mitawi alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa
Baraza hilo.
Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa kutoka kundi la jamii ni
pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa cha UDSM, Prof. Bernadetha
Killian, jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Juston Mlay na Mhandisi wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Mfanyabiashara maarufu Bw. Ali
Mufuruki.
Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa kutoka Tasnia ya Habari ni pamoja
na Rose Mwalimu Haji, Tuma Abdallah kutoka Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN),
Mkuu wa Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la The Guardian,
Warrace Maugo.
No comments:
Post a Comment