Mama Salma Kikwete |
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi
wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye zoezi la
kuipigia kura Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwishoni mwa mwaka huu.
Mwito
huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete
wakati akiongea na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika
katika tawi la Msinjahili wilayani humo.
Mama
Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema zoezi
la uandikishaji litafanyika kwa muda wa wiki moja na katika mkoa huo
litaanza tarehe 16 hadi 22 mwezi huu hivyo basi ni muhimu wananchi
wakajitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha.
“Mkoa
wetu ni mmoja kati ya mikoa minne ya mwanzo itakayoanza zoezi hili,
mikoa mingine ni Mtwara, Ruvuma na Njombe. Ni muhimu wananchi
mkajitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani uandikishaji utafanyika kwa
njia ya mashine na baada ya wiki moja mashine hizi zitahamia katika
mkoa mwingine”, alisema Mama Kikwete.
Kuhusu
Katiba inayopendekezwa alisema ni ya watanzania wote kwa maendeleo yao
kwa kuwa inamgusa kila mtu. Ili wananchi waweze kuipigia kura ni muhimu
wakajiandikishe katika daftari la kudumu la wapiga kura na ifikapo
tarehe 30 ya mwezi wa nne mwaka huu wakaipigie kura ya Ndiyo.
Aidha
MNEC huyo alisema Tanzania yenye neema inawezekana kwani maisha bora ni
kuhakikisha binadamu anafunguka kiakili kwa kupata elimu kwa kuona
umuhimu wa hayo yote Serikali imejenga shule nyingi za Sekondari za Kata
ambazo zimeweza kuwasaidia watoto wengi kutoka familia maskini kupata
elimu jambo ambalo halikuwepo katika miaka ya nyuma.
Mama
Kikwete anasema, “Hivi sasa huduma za afya zimeboreshwa na zinapatikana
kirahisi ukilinganisha na miaka ya nyumba kwani Serikali imejenga
Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali, idadi ya wafanyakazi katika sekta
hii imeongezeka na vifaa tiba pamoja na madawa vinapatikana.
“Barabara
zimejengwa kwa kiwango cha lami katika maeneo mengi nchini na hivyo
kurahisisha usafiri, wananchi wanasafirisha bidhaa zao kutoa eneo moja
hadi lingine haya ndiyo maendeleo kwani mkulima analima mazao yake na
kuwa na uhakika wa kuyafikisha sokoni kwa mnunuzi na walaji”,.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi Mzee Alli Mtopa aliwasihi
wanachama wa Chama hicho kuondoa tofauti zao za makundi ya wagombea
waliyokuwa nayo katika uchaguzi uliopita bali waungane na kuwa kitu
kimoja na kufanya kazi za chama kwa kufanya hivyo watapata ushindi wa
kishindo katika uchaguzi ujao.
Mzee
Mtopa alisema vyama vya upinzani vinaona maendeleo yaliyofanywa na
Serikali ya CCM lakini havitaki kukubali ukweli bali wanapita mitaani na
kuwarubuni watu kuwa hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika jambo ambalo
siyo sahihi na kuwataka wananchi hao kuwapuuza na kuendelea kufanya
kazi ili wajiletee maendeleo.
Mama
Kikwete pia alifanya vikao na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya
Chama hicho katika matawi ya Sheikh Badi, Msonobari na Msinjahili
alizungumza nao mambo mbalimbali yanayohusu kazi za chama hicho na
kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Akiwa
katika tawi la Msonobari alikipatia kikundi cha utengenezaji batiki cha
wanawake wa mtaa wa Msonobari juu na chini shilingi laki tano ili ziweze
kuwasaidia kununua vitendea kazi na malighafi kwa ajili ya uzalishaji
wa batiki.
No comments:
Post a Comment