Tangazo

February 11, 2015

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI IDODI 'AMKIMBIA' MBUNGE WA CHADEMA


 Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema CHIKU ABWAO akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto.
 Mbunge  Chiku Abwao akiwa katika eneo la nje ya jengo liloungua.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Mbunge wa viti maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao alisikitiswa na uongozi wa shule  ya sekondari ya Idodi kushindwa kumpokea kama mbunge na mama aliyeguswa na ajali ya moto katika shule kwa kuwa alikuwa ameshatoa taarifa kabla hajaenda katika shule hiyo.


Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wanahabari wa manispaa ya iringa waliokuwa wameongozana na mbunge huyo walikasilishwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa shule ya sekondari ya Idodi na walianza kuhoji je? angekuwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na waziri au mbunge wa jimbo hilo wangemfanyia hivyo.

Licha ya hujuma alizopewa ambazo zinasadikika kuwa za kisiasa mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Chiku Abwao aliendelea na zoezi lake la kutoa msaada wa shilingi milioni moja ili kusaidia majukumu mengine ya shule hiyo kutokana tathimini fupi iliyotewa na baadhi ya walimu.

Akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule, alisema kuwa ameguswa na ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada huo.

Aidha Abwao aliishauri serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida ili kuwawezesha  wanafunzi kuishi kumi katika bweni moja tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanaishi zaidi ya mia na ishirini katika bweni moja.

Alisisitiza kuweka ulinzi mzuri kwenye mabweni kwa kuwa suala kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika shule hiyo na kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni ya shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.


Alipotafuta mkuu wa shule kwa njia ya simu na kuulizwa kwanini umemkimbia mbunge alijibu kwa kusema kuwa alikuwa na majukumu mengine kwa hiyo sio lazima kumpokea mbunge wakati kuna majukumu mengine makubwa zaidi ya yeye.

No comments: