Tangazo

August 19, 2015

Airtel yatoa Mikopo kwa Mawakala wa Airtel Money

Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi (kulia) na Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks  wakionyesha bango kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks, Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi na Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks na Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi. 
Baadhi ya mawakala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Mkopo kwa wakala, huduma itakayowawezesha kupata mikopo isiyo ya dhamana kupitia huduma ya Airtel Money.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

*Mikopo isiyo na dhamana
*Zaidi ya mawakala 20,000 kunufaika


Dar es Salaam, Jumanne 18th Agosti 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Afb Tanzania imezindua huduma ya mikopo kwa wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama "Timiza Mkopo kwa Wakala",
itakayowawezesha  mawakala wa Airtel Money nchini nzima kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia shilingi 50,000 hadi 500,000.


Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mkuu wa Biashara Airtel , Bwana Arindam Chakrabary alisema" Airtel inatambua kuwa mawakala wetu wanatafuta fursa ya kukuza biashara zao na kuongeza mitaji. Na leo tunayo furaha kuzindua huduma ya kwanza Tanzania na Afrika "Timiza Mkopo kwa Wakala" mikopo isiyo na masharti mahususi kwa mawakala wetu.

Huduma hii ya mikopo kwa mawakala  itawanufaisha mawakala zaidi ya 20,000 nchi nzima,  na tunaamini mikopo hii itasaidia kukuza biashara za mawakala wetu , kuwaongezea faida zaidi na hatimaye kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha" Chakrabarty aliongeza kwa kusema" Mwaka jana tulizindua huduma ya Timiza kwa wateja wetu nchini nzima,  ambayo kwa sasa ina zaidi ya wateja milioni 7 wanaoweza kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti kwa urahisi , mikopo ambayo inawasaidia kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.


"Timiza Mkopo kwa Wakala" itatoa kwa mawakala wetu wa Airtel Money uhuru wa kupata mikopo ya  haraka isiyo na masharti bila kupitia njia ndefu zakupata mikopo katika mfumo wa kawaida. Tunaamini huduma hii inatasaidia na kuwawezesha mawakala wa Airtel Money kupata fedha za kutatua mahitaji yao ya muda mfupi na mrefu wakati wote.

Aliongeza Naye Msimamizi  Mkuu Afb Tanzania, Rwebu Mutahaba, amesema " Mawakala wanapata mikopo kulingana na matumizi yao ya simu ndo mana tumeweza kuwaamini na  kuwapatia mikopo isiyo na masharti. 

Lengo kubwa ni kuwapatia watu fulsa ya kupata huduma ya kisasa na kibunifu ambayoa haijawahi kutolewa kabla.  Afb Tanzania tunajivunia ushirika huu na Airtel ambao umetuwezesha kutoa suluhisho kwa wateja wa Airtel, mikopo kwa mawakala ni moja ya huduma nyingi za kibunifu tulizonazo na tunazopanga kuzindua katika mienzi ijayo nchini Tanzania".

"Timiza Mkopo kwa Wakala" ina viwango na riba tofauti zenye marejesho ya ndani ya siku saba, wiki mbili au mwezi mmoja . Kiasi cha kukopa kitategemeana na matumizi simu ya wakala na jinsi anavyorudisha mkopo wake kwa wakati. Mteja atakapo rudisha mkopo wake ndani ya siku 7,14 au 28 mojakwamoja atawezeshwa kupata mkopo mwingine. Inachukua dakika moja kwa mteja kujaza fomu ya kuomba mkopo kupitia simu yake  na kasha mara baada ya kujaza pesa zinawekwa kwenye akaunti yake ya Airtel Money hapohapo". alisema Mutahaba.

Kwa upande wake, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha, Bwana Ridhiwan Masudi alisema"  sisi kama Serikali tumefurahishwa na hatua walioichukua Airtel katika kuboresha mfumo rasmi wa kifedha kupitia huduma ya Airtel Money.  Tunafurahi  kuona huduma ya Airtel Money  ikikuwa kwa haraka na kuwafaidisha watanzania wakawaida hususani wanaoishi katika maeneo ya pembe zoni mwa nchi.


Napenda kuchukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kuleta bidhaa na huduma za kibunifu ili kuweza kuipatia jamii huduma bora za mawasiliano na kukuza zaidi huduma za kifedha."



Mawakala wa Airtel Money wanaweza kujipatia mikopo kwa kupiga *150*60#, na kuchagua 4  ili kupata orodha ya mikopo kwa wakala , na kisha kuingiza namba ya simu na namba ya siri  na baada ya hapo wataunganishwa kwenye orodha ya mikopo ya Timiza.

No comments: