Tangazo

September 18, 2015

KUMBUKUMBU YA MIAKA 8 YA BABA MZAZI WA BLOGGER FATHER KIDEVU NA BIRTHDAY YA FATHER KIDEVU

Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007)

Mroki Mroki-Father Kidevu
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika nane sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki 'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan  pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako. 

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

No comments: