Tangazo

November 2, 2015

MMLIKI WA FM ACADEMIA, MARTIN KASYANJU AFARIKI DUNIA

TASNIA ya Muziki wa Dansi nchini, imepata pigo kufatia kifo cha mmiliki wa Bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”, Martin Kasyanju (Pichani) aliyefariki dunia jana. 


Msemaji wa FM Academia, Kelvin Mkinga amethibitishia kifo cha Martin aliyefariki katika hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu kwa siku kadhaa. 

Kelvin amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria, lakini baadae ikagundulika ana ‘pneumonia’ (nimonia) pia.  

Kelvin amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu, Oysterbay Mtaa wa Mahenge jijini Dar es Salaam.

No comments: