Tangazo

July 11, 2016

MHE. MAVUNDE AWAASA VIJANA KUACHA KULALAMIKIA AJIRA WAKATI UWEZO WA KUJIAJIRI WANAO

Picha/Habari na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde Jumamosi hii amekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kujadili changamoto za ajira nchini lililoandaliwa na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM na kuwahusisha wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu mbalimbali nchini.
Akiongea kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, mheshimiwa Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao.
Mhe. Mavunde alisema kwa sasa mambo yamebadilika sana hivyo watoe fikira za kumaliza chuo na kujiwekea fikra za kuajiliwa wakati wao wenyewe wanaouwezo wa kutengeneza ajira kutokana na mambo watakayobuni kufanya.
Alisema kuwa kwa sasa vijana wanayonafasi ya kubuni miradi na serikali ikawasaidia kuiendeleza mbele kwa kuwapa mitaji ili waifanikishe.
"Vijana acheni Kulalamikia ajira, zama za mababu zetu ajira zilikuwa za kutosha ila kwa sasa kila mmoja akimaliza chuo akataka aje apate ajira serikalini haiwezekani, hivyo nawaasa kujiwekea malengo ya kujiajiri wenyewe ili muingine katika soko la ushindani," Mhe. Mavunde.
Pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu wa muda. “Muda ni kitu cha msingi na kukitunza sana,” alisema.
“Nilikuwa na ndoto ya kuja kuitumikia jamii, nilikataa kazi nyingi za kuajiriwa ili kuifuata ndoto yangu, nilikuwa naamini maisha yangu yapo kwenye siasa, mpaka sasa niliitambua njia yangu na ndio njia niliyopitia,” alisisitiza.
Kwa upande wake MC Pilipili ambaye pia alikuwa mmoja wa wazungumzaji, alisema kuzaliwa kwenye familia maskini hakumaanishi kuwa huwezi kujinasua na kuwa na maisha unayotaka.
“Usikasirike kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni kujiondoa katika umasikini,” alisema mchekeshaji huyo ambaye pia ni mtangazaji wa kituo hicho cha redio.
“Mungu kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika maisha yako, usifate mkumbo, niliamua kukifata kipaji changu katika kuchekesha.”
Msimamizi Mkuu wa Radio TimesFM, Ron Fidanza akiwapa amasa vijana kusoma kwa bidii.
Naye Msimamizi Mkuu wa Radio TimesFM, Ron Fidanza aliezea mchango wa kipindi cha Campus Vibes kwa wanafunzi wa chuo: Times Fm imejikita kutoa mchango wake kupitia kipindi cha Campus Vibes ili kujenga jukwaa la mazungumzo kwa vijana na wanafunzi wa elimu ya juu,” alisema.
“Pia Times Fm imeanzisha program maalum ili kuwawezesha wasomi wa habari vyuo vikuu kufanya mazoezi kwa vitendo.”
 
Mkurugenzi wa kampuni ya Maznat Bridal, Maza Sinare akiongea na katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
Mhadhiri wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akiwaasa vijana kuacha kulalamika wajitume ili waweze kujikwamua kimaisha.
Mhariri Mkuu wa TimesFm, Zorha Malisa akiwashukuru wanafunzi kwa kuja.
BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
Mkurugenzi msaidizi wa Tanzania Patriotist Network (TAPANET) akielezea changamoto zinazowakabiri vijana.
Mwanafunzi wa UDSM, Eze Bernard akimuuliza swali Naibu Waziri Mhe. Mavunde.
 Mwanafunzi wa DIT, Neema Pambe akiuliza swali.
Wanafunzi wakipata ukodak na Maibu Waziri Mhe. Mavunde.
Nilipata ukodak na Mhe. Mavunde na Mc Pilipili mara baada ya kumaliza kongamano. Nikiripoti kutoka eneo la Tukio ni Mimi Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog (kwanza kulia)..

No comments: