Benki ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki na huduma endelevu za kimaendeleo kwa wateja wake.
Zaidi ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza fedha, jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu , jinsi gani taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za mtu binafsi zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi zinapatikana kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Kwa kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na kilimo Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa bidhaa zinazo zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya tafiti mbalimbali nchi nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo maalumu kwa wajasiriamali wadogo na wakati,
kuzisaidia taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa misitu kwa pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na kuwaunganisha wanachama na fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa kimataifa. Akiongea kwenye warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa KCB Bwana Godfrey Ndalahwa alisema kwamba, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi. “ Dhumuni letu sio kutoa suluhisho yakinifu kwa masuala ya kibenki tu bali pia ni kuwapa ujuzi na nyenzo zinazohitajika katika kufanikisha biashara zao” Wanachama wa KCB Biashara club watapatiwa ujuzi wa kutosha kupitia warsha mbalimbali ambapo ushauri wa kibiashara utatolewa kutoka kwa wataalam waliothibitishwa.
Warsha hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kuwa kwenye mtandao na kuwasiliana wao kwa wao na kushirikishina ujuzi bora wa kibiashara. Katika kuongezea hili, pia wanachama watapata fursa ya kusaidiwa na mameneja uhusiano wanaowasikiliza kwenye mahitaji yao ya kifedha. Wanachama wa KCB Biashara club pia watanufaika na fursa zilizopo nje ya nchi ambapo matawi ya benki za KCB yapo.
“ Ikiwa ni moja ya maidhinisho yanayotolewa na club hii, tumeweza kupata maelezo kutoka kwa mtendaji wa KCB Biashara club Bwana Moses Odipo ambaye ametushirikisha safari za kibiashara za mwaka 2017. Hii itawawezesha wanachama wetu kushiriki kwenye safari za mkoa mpaka safari za kimataifa katika kuwezesha biashara zao.Wanachama watahudhuria maonesho ya kibiashara ya Kimataifa ili kujifunza jinsi wajasiriamali wengine wa kiwango chao wanavyo jiendesha kwa dhumuni la kuboresha biashara zao .
Wakati akitoa mchanganuo wa KCB Biashara Club, Bwana Masika Mukule, mkuu wa kitengo cha wateja masuala ya kibenki, alisema kwamba, Biashara club imedhamiria kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwapa nyenzo na kuhakikisha wana ujuzi sahihi wa kuendesha biashara zao na kutoa dondoo juu ya taarifa za kifedha zinazohitajika na taasisi za kifedha pindi wanapo omba mkopo.
“Mwaka huu warsha yetu ina maudhui mazuri sana yaliyoandaliwa kwa kufuata maoni yaliyotolewa kwenye warsha yetu ya mwaka jana na tunaamini mwakani tutakuwa tumewawezesha baadhi ya wajasiriamali wadogo na wakati kufikia kiwango cha wateja wa kiwango cha juu.Bwana Mukule aliendelea kusema kwamba KCB wanazo bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la wajasiriamali wadogo na wakati ikiwa ni pamoja na Masharti ya mkopo, overdaft facilities, Overdraft facilities, Bank Guarantees, Invoice Discounting, Documentary letters of Credit, Asset Based Finance na Bills Discounting.
Mbali na hizi kitengo hiki kinatoa mikopo ya nyumba kwa wanao nunua, matengenezo au kumalizia ujenzi, Advantage Banking na bidhaa za kibenki kwa wateja wetu waliopo nje na ndani ya nchi .Wanachama wetu wana mengi ya kupokea kutoka kwetu,” Alimalizia Bwana Mukule
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KBC, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam. Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Edgar Masatu akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
No comments:
Post a Comment