Tangazo

March 20, 2017

KONGAMANO LA MAADILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

 Naibu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano la maadili litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa kuanzia saa nne asubuhi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inatarajia kufanya kongamano  linalolenga maadili kwa Taifa nchini.

Kongamano hilo litafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa wizara hiyo,  Anastazia Wambura amesema ni wajibu  kwa kila mwanajamii kuthamini, kuenzi na kuendeleza maadili mema, mila na desturi zinazofaa.

“Serikali hususani wizara inajukumu la kutoa muelekeo na usimamizi kuhakikisha Taifa linaenzi na kuimarisha utambulisho wake na kujenga utamaduni huru na sio huria” alisemaWambura.

Aidha Wambura alisema kuna fursa ya kubaini, kuenzi na kukuza, kuhifadhi  na kurithisha utamaduni na sanaa vyenye kuzingatia na kuimarisha maadili, mila na desturi kwa kuleta maendeleo.

“Wananchi wamekuwa  wanaendelea kujihusisha  na shughuli mbalimbali za Kifani, Sanaa na utamaduni ikiwemo ngoma za asili, filamu, muziki, jando, unyago, matambiko, Sherehe na maadhimisho mbalimbali” alisemaWambura.

Ameongeza kuwa shughuli hizo ni halali ilimradi zifanywe  kwa kuzingatia sheria na kanuni na msingi wa asili yake, kwa maana kwamba kama jambo ni la faragha na usiri libaki kwenye uhalisia wake na kuhusisha rika jinsia na asili yake.


No comments: