Na Mathias Canal, Zanzibar
Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference)
limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao
350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji
kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.
Diaspora
wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya
kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania
kuwa nchi ya viwanda.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa
Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili
Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha
Kama Wilaya ya Magharibi A.
Mhe Makamba
alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia
vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama
wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.
Alisema kuwa
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto
nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na
kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea
kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.
Changamoto
zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba
alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia
kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema serikali
itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya
uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji
katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio
nchini na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa
Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu
katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi
na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana
kukua siku hadi siku.
Alisema kuwa
fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo
vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo
zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa
chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea
fedha hizo.
Aidha, Alisema
kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato
ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba
aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili
kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata
sheria na taratibu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.

Kongamano hilo
ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015
Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.
Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.
Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa
pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi
sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na
ushirikiano bora kati yao na serikali.
Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,
Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB)
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya
nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibarBaadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni
(4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi
Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni
(4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya
nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi
katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya
nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB)
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya
nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
No comments:
Post a Comment