Tangazo

May 22, 2018

Ziara ya Kinana Afrika Kusini

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akimkabidhi Rais wa Chama Cha Ukumbozi wa Afrika Kusini (ANC) Rais wa  Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa barua maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg, jana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu Mkuu wa ANC Ace Magashule Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Rais wa ANC Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa ANC Gwede Mantashe, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa ANC, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Katika ziara hiyo ambao Kinana ameambatana na Wenyeviti wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi, ina lengo la kuendeleza uhusiano na mshikamano uliopo bana ya Vyama hivyo.

No comments: