Tangazo

September 13, 2011

Dua maalum ya kuwaombea wananchi waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander

Viongozi wa kitaifa kama wanavyoonekana kwa pamoja na  wananchi wa Zanzibar wakiitikia dua maalum iliyoombwa katika Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar jana kwa wananchi waliopoteza roho zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,na kuwatakia maghufira kwa Mwenyezi Mungu,kuwasamehe makosa,kuwaweka makazi mema Peponi Ameen. Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi wakati wa Dua maalum ya kuwaombea wananchi waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar na kuwataka kuwa subira kwani hayo yaliyotokea ni rehma za Mwenyezi Mungu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,wakati wa Dua maalum ya kuwaombea wananchi waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

No comments: