Tangazo

September 13, 2011

TASWA YATUMA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI YA MELI ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando
 

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutokana na vifo vilivyotokea vya watu zaidi 200 baada ya kuzama kwa meli ya ya Mv Spice Islander mwishoni mwa wiki Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 TASWA inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu, huku tukiwaombea waliofariki Mwenyezi Mungu ahifadhi roho zao mahali pema peponi na wale majeruhi awape nguvu wapone haraka waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

Tunaziomba familia zilizopoteza ndugu zao ziwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na waamini kwamba huo ni msiba wetu sote na si wao peke yao.

TASWA inaamini wapo wanamichezo waliopoteza maisha kwenye meli hiyo na pia wapo wanamichezo waliopoteza ndugu na jamaa zao, wote tunawapa pole na wawe na moyo wa subira.

Imetolewa na:
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
13/09/2011

No comments: