Wizara ya Maliasili na Utalii inautaarifu umma kuwa mchakato wa kupitia maombi ya vitalukwa kipindi cha 2013 – 2018 umekamilika na kuwa kampuni 60 zitagawiwa vitalu.
Kampuni zitakazogawiwa vitalu ni kwa uwiano ufuatao:-
i. Kampuni za kitanzania zitakazogawiwa vitalu ni 51 kati ya 60
(sawa na asilimia 85% ya kampuni zote);
ii. Kampuni za kigeni zitakazogawiwa vitalu ni 9 kati ya 60
(sawa na asilimia 15% ya kampuni zote);
iii. Kampuni 15 zitapewa kitalu kimoja kwa kuzingatia maombi yao. Kati ya kampuni hizo, kampuni 1 ni ya kigeni
(sawa na asilimia 2% ya kampuni zote) na 14 ni za kitanzania (ambayo ni asilimia 23% ya kampuni zote);
iv. Kampuni zenye vitalu vingi, yaani vitalu 4 hadi 5 ni 13, ambayo ni sawa na asilimia 22% ya kampuni zote);
Aidha, kuna vitalu 14 ambavyo havijapata waendeshaji, 10 havijaombwa kabisa hata baada ya kutangazwa mara ya pili, na 4 vimeombwa mara zote mbili na waombaji wasio na sifa kabisa kisheria. Hivyo, serikali inatafakari namna ya kuviendeleza na kuviendesha vitalu hivyo ambavyo vingi rasilimali zake zimepungua sana kutokana na uvamizi wa wananchi kwa shughuli za kilimo, makazi na hata ufugaji. Kwa kuwa Kampuni za uwindaji za kigeni, kwa mgao huu, tayari zimeshafikia ukomo wa asilimia 15%, hii ni fursa kwa wawekezaji wapya, hasa watanzania kuleta maombi vitalu hivyo vitakapotangazwa.
2.0 SHERIA ILIYOTUMIKA
Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Wanyamapori, pamoja na mambo mengine, imekuwa ikisimamia matumizi ya wanyamapori ambayo ni matumizi ya uvunaji (consumptive utilization) na matumizi yasiyo ya uvunaji (non consumptive utilization) kupitia kifungu 38 cha sheria ya Wanyamapori na.5 ya Mwaka 2009 (sura 283). Mojawapo ya matumizi ya uvunaji ni Biashara ya Uwindaji wa kitalii, biashara ambayo imekuwa katika uendeshaji na usimamizi wa sheria tofauti tangu 1934.
Usimamizi wa Biashara ya Uwindaji wa kitalii kwa muda mrefu umekuwa ukifanywa zaidi na Makampuni ya kigeni na wateja wao wengi walitoka nje. Kabla ya sheria mpya, sheria Na.12 ya mwaka 1974 na kanuni zake ndizo zilizokuwa zikitumika. Hata hivyo, kumekuwepo mapungufu kadhaa katika mfumo uliokuwa ukitumika ambao ulisababisha malalamiko mengi toka kwa wadau wa sekta hii. Hivyo, sheria ya Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 ililenga kurekebisha mapungufu hayo.
Kufuatia matakwa hayo ya kisheria, maandalizi yafuatayo yalifanyika kati ya 2008 hadi Januari 2011:-
i. Kupitia upya vitalu vyote kwa lengo la kuvigawanya ili kuongeza washiriki na mapato kwa kuzingatia ukubwa, ubora (kama vile wingi na aina za wanyama, uwepo wa maji na malisho, miundombinu ya eneo). Kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na kukamilika Desemba 2010.
ii. Kuandaa kanuni zitakazoweka, pamoja na mambo mengine, vigezo vitakavyotumika kufanya tathmini kwa waombaji wa vitalu. Kazi hii ilikamilika Julai 2010.
iii. Kuteua wajumbe wa kamati, kazi ambayo ilikamilika Machi 2011. Wajumbe wafuatao waliteuliwa kwa mujibu wa Kifungu 38 (3) cha Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya 2009: Kwa taarifa zaidi:BOFYA HAPA

No comments:
Post a Comment