Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika
Machi 1, 2015 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro zimepata msisimko mpya baada ya
wanariadha nyota wa Tanzania kuthibitisha kushiriki.
Mkurugenzi wa Mbio hizo, John Bayo jana katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari aliwataja baadhi ya wanariadha nyota kutoka Tanzania kuwa ni
Andrew Sambu, Daudi Joseph, Mashaka Masumbuko, watachuana na wanariadha wengine
kutoka nchini na kutoka nje ya nchi katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager
Marathon kwa wanaume za kilometa 42.195.
Kwenye upande wa marathon wanawake Fabiolla William, Sarah Maja
and Banuelia Katesigwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania watakaochuana na
wenzao kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwania tuzo mbalimbali kwenye Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanawake za Kilometa 42.195.
Aidha, wanariadha Fabian Fabian Joseph, Alphonce Felix, Dickson
Marwa wamethibitisha kushiriki Tigo Kili Half Marathon wanaume wakati Mary
Naali, Natalia Elisante, Catherine Lange na Jacqueline Sakilu ni miongoni mwa
majina maarufu katika riadha yaliyothibitisha kushiriki kupitia kundi la
wanawake litakalochuana katika Mbio za Tigo Kili Half Marathon.
Katika mbio za nusu marathon ambazo Tanzania ina historia ya
kufanya vizuri, Fabian Joseph ana rekodi ya ushinda Kilimajaro Marathon mwaka
2010 ambapo alimaliza mbio katika muda wa 1:3;59 na vilevile ana rekodi ya
kushinda Edmonton Marathon mwaka 2005 kwa muda wa 1:01:08.
Akiwa ametengeneza rekodi nyingi, Mary Naali ni kati ya wanariadha
bora nchini katika mbio za kilomita 21 maarufu kama Half Marathon. Alishinda
Vienna Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza katika muda wa 1:12:16 na baada ya
hapo akavunja rekodi kwenye mbio za kilomita 25 za Arusha VIP Race mwaka 2011
ambapo alishinda kwa 1 1:20:52 na kuvunja rekodi ya 1:22:18 iliyokuwa imewekwa
na Josephine Deemay mwaka 2006. Mei mwaka 2013 pia alishinda mbio ya Bucharest
International Marathonihuko Romania akimaliza katika muda wa 1:16:32.
No comments:
Post a Comment