Tangazo

September 21, 2011

HAWA NDIO VIONGOZI WETU WA KISIASA!

Mh. Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Dk. Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa ilikuwa kwenye shughuli moja inayohusu CCBRT.

Mh Dk. Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mh. Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi - CUF Tanzania.


Watanzania wenzangu wanasiasa wetu wanapokua wanakuja kutuomba kura, wanakuja na mengi sana kutoka kwenye vinywa vyao, ni vema yale wanayoyasema tuyachukulie kama vile tunawaona wako pamoja wamekaa meza moja wakiwa wanatueleza hayo ya kwao. Hili litatusaidia sana kuwafanya wao wasiweze kutugombanisha sisi mpaka kutupelekea kutokea yale ambayo hatutaki yatokee.
Kwa hisani ya Kapingaz Blog

No comments: