********************************
Michuano ya fainali ya kitaifa ya vijana wenye umri U-17 maarufu kama Airtel Rising Stars, imeendelea kutimua vumbi hapo siku ya Jumapili, ambapo timu ya Dar es Salaam imetoa onyo kali kwa timu shiriki baada ya kuichapa timu ya Iringa 10-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume.
Mechi hiyo ilikuwa ni muendelezo wa michuano hiyo ambayo ilianza Jumamosi kwa timu ya Morogoro kuichapa Mwanza 6-0.
Katika mchezo wa Jumapili, dalili za timu ya Dar es Salaam kuibuka na ushindi mnono zilianza mapema ambapo dakika tano za mwanzo wa mchezo huo, washumbuliaji wa Dar es Salaam walikuwa washafika langoni la wapinzani wao mara tatu huku kipa wa Iringa akifanya kazi kubwa kuzuia mashuti makali yaliyokuwa yakielekezwa langoni mwake.

Hata hivyo, katika dakika ya 10, Dar es Salaam walianza sherehe ya mabao baada Rajabu Mwarami kuandika bao la kwanza. Mnamo dakika ya 22 Omary Abdallah aliipatia Dar es Salaam bao la pili na kabla wachezaji wa Iringa hawajakaa vizuri, Shaban Mtambo akaongeza bao la tatu dakika ya 24.
Joseph Seleman alifunga goli la nne dakika ya 38 na mpaka timu zinakwenda mapumziko, timu ya Dar es Salaam ilikuwa inaongoza kwa mabao manne.
Mnamo dakika ya 58 ya kipindi cha pili, Joseph Seleman ailiendeleza karamu ya magoli baada ya kufunga goli la tano. Dakika ya 69 Omary Abdallah aliongeza goli la sita. Timu ya Iringa, ambayo kwa hakika walionyesha kuchoka kabisa, waliendelea kuruhusu nyavu zao kutikizwa dakika ya 72 mfungaji akiwa ni Rajabu Moto na kabla dakika tatu baadaye Alphonce Mkunde alifunga goli la nane. Goli la tisa na kumi yalifungwa na Amos Nguti na Abdalatif Hamis.
Michuano hiyo ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Klabu ya Manchester United ya Uingereza inaendelea tena hapo Jumanne ambapo Morogoro watacheza na Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment