Tangazo

September 19, 2011

"MOTO TENA MBEYA" SOKO DOGO LA FOREST MAGHOROFANI LATEKETEA KWA MOTO

Moto wateketeza soko hilo lililopo Forest ya zamani karibu na Chuo cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria Jijini Mbeya.
Moto ulianza majira ya saa 9:00 kamili usiku juzi na Zimamoto walifika saa 9:10 na kufanikiwa kudhibiti moto huo ambao umeteketeza vibanda kadhaa na kusababisha hasara kubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evans Balama asaidia kuzima Moto huo, lakini wadau wanajiuliza kunani katika masoko ya Mbeya na kwanini tahadhari hazichukuliwi?
Mtandao huu umefanikiwa kukuta baadhi ya masalia ya vibanda yakifuka moshi. Picha zote kwa hisani ya Latest News Tz

No comments: