Tangazo

September 19, 2011

TPA YAZINDUA BOTI ZA DORIA IKIWA NI MAADHIMISHO YA MIKA 50 YA UHURU KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI

Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Omari Nundu (kushoto) baada ya kuzindua boti 4 za doria majini  katika bandari ya Dar es Salaam Sept 16.2011, akiwa na Naibu wake, Mhandisi Athmani Mfutakamba (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Mhandisi Omari Chambo (kulia). Uzinduzi huo ni katika Maadhimisho ya Miaka50 ya Uhuru kwa Wizara ya Uchukuzi. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO 
Sehemu ya wafanyakazi wa TPA wakifuatilia kwa makini tukio hilo.
Kweli Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza! Mwanamke pekee Mhandisi Marine TUG, Maisara Rumani (katikati) akiwa kwenye meli ya NYANGUMI , akiwa na Mhandisi Sifuel Felix (kushoto) pamoja na Mhandisi Nicholus Mfumgomara.
Meneja Mawasiliano wa TPA, Frakline Mziray (kulia) akiwa na msanii mkongwe wa muziki nchini, Mzee Muhidini Ngurumo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athmani Mfutakamba (kushoto) akizindua eneo la ujenzi wa kutunzia makontena (Gerezani Creek Container).  Pichani Mwengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omari Chambo (suti nyeusi.
Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nyundo (katikati) akizindua huduma kwa mteja kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania. Kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe.  Kutoka (kulia) ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athumani Mfutakamba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omari Chambo.
Hizi ndizo boti zilizozinduliwa  katika Bandari ya Dar es Saalam na Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Omari Nundu (hayupo pichani). Boti kubwa 2 ni za kuongoza meli na ndogo kwajili ya kuwapeleka manahodha na kufanya doria.

No comments: