Siku nyingine kitoweo cha samaki huadimika kutokana na hali ya hewa kuchafuka baharini basi huwa zinasimama hali inayopelekea watu kuuchapa usingizi tu. |
Siku nyingine mambo huwa mazuri. |
na wakati mwingine mambo huwa mswano...... |
lakini pia pembezoni mwa soko hilo huwezi kuwakosa wachapa usingizi katika ufukwe wa bahari ya Hindi wenye upepo mwanana... masaa yooote wao ni usingi tuuuu... |
Kinamama wajasiriamali hawakosekani... kama hawa wakipaa samaki baada ya kuwanunua kwenye mnada na kisha huwakaanga tayari kwa kwenda kuwauza reja reja mitaani yaani 'Uswazi' |
haya hapo mimi sisimulii kitu utaja mwenyewe... |
we mama nunua samaki mimi najisevia pweza huku... |
Miundombinu ya Soko la kukaangia samaki bado ni utata kwani moshi unawumiza sana wafanyabiashara wa humo. |
Feri hakuna mambo ya Barber Shop... eti sijui niweke Black, ooh mara Magic ooh eti Scrab sijui la hasha kule ni kipara cha wembe kwa kwenda mbele... |
No comments:
Post a Comment