Tangazo

June 19, 2012

Kampeni ya Polisi ya Utii wa Sheria bila Shuruti: Mzee Mwinyi azindua Vitabu vya Utii wa Sheria ni Dhawabu na Baraka za Utii

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (katikati) akizungumza na viongozi wa Dini za Kikristo na Kiislamu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Utii wa Sheria bila Shuruti ulioambatana na uzinduzi wa vitabu vya 'Utii wa sheria ni thawabu pamoja na Baraka za Utii' uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 19.12. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na 9kulia) ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.(Picha na Jeshi la Polisi)

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi vitabu vya Utii wa Sheria ni Dhawabu na Baraka za Utii,   Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum baada ya kuvizindua.Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipetenkoste,  Askofu Daniel Aweti.(Picha na Jeshi la Polisi)

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja (wa pili kushoto) akiwa pamoja na viongozi wa dini za kiislamu na kikirsto wakifuatilia kwa makini hotuba wakati wa uzinduzi wa Vitabu vya Utii wa Sheria ni thawabu pamoja na Baraka za Utii vilivyozinduliwa  na RaisMstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.(Picha na Jeshi la Polisi)

No comments: