Tangazo

June 16, 2012

KIJANA JACKSON THOBIAS a.k.a KUSH ALIYEGONGWA NA TRENI


Na Mwandishi wetu. 
Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao Kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza 'music kwa headphones' huku 'akichati katika simu yake' wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliyeshinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends Mei 12 .2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Ame
n.

No comments: