Tangazo

June 14, 2012

Nape aanza Ziara Mkoani Iringa

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye ameanza ziara ya kikaz i ya siku nne mkoani Iringa, ambapo atakagua uhai wa Chama na kukiimarisha katika wilaya mbali mbali mkoani humo. Kufuatia ziara hiyo Nape leo amewasili mjini Mafinga katika wilaya ya Mufindi kuanza ziara hiyo.PICHANI:  Ofisi ya CCM wilaya ya Njombe iliyopo mji i Mafinga. (picha zote na Bashir Nkoromo)

Vijana  Erick Anthony na Emmanuel  James wakicharaza ngoma wakati Nape alipowasili, Ofisi ya CCM wilaya ya Mafinga iliyopo mjini Mufindi.

Nape akisalimia wanafunzi wa Chuo cha Uhazli Njombe, baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya Mafinga wilayani Mufindi.

Vijana wa CCM wakiimba wimbo wakati wa mapokezi ya Nape (kushoto) ofisi ya CCm wilaya ya Mafinga, wilaya ya Mufindi.

Katibu Mwenezi Kata ya Halimba, Mafinga, Lupumko Mandele (koti la pink) akihamasisha kwa kucheza mbele ya Nape katika mkutano wa ndani mjini Mafinga.

No comments: