Tangazo

June 18, 2012

Timu ya soka ya Benki ya NBC yaichachafya timu ya Barclays.

Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Hussein Shabani (kulia) akigombea mpira  na Henry Justin wa timu ya Barclays katika mechi ya kirafiki  iliyofanyika jijini Dar es Salaam. NBC ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Mkurugenzi wa Teknolojia Habari wa Barclays, Dakshit Pandya (katikati) akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa nahodha wa timu ya soka ya Benki ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wao wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Technolojia Habari (IT) wa NBC, Pete Novat.

Mkuu wa Idara ya Teknolojia Habari (IT)  wa Benki ya NBC,  Pete Novat(kulia) akikabidhi kikombe cha ushindi wa pili kwa nahodha wa timu ya soka ya Barclays, Siaga Mgweno mara baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu za benki hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. NBC ilishinda kwa penalti 4-3. Katikati ni Mkurugenzi wa IT wa Barclays, Dakshit Pandya.

Wachezaji wa timu ya soka ya NBC wakishangilia baada ya kuibuka kidedea kwa kuinyuka timu ya Barclays kwa mabao 4-3 katika mchezo wa soka wa kirafiki jijini Dar es Salaam.

No comments: