Kipindi cha Kambi Popote kinachorushwa Clouds Tv kitaungana na Lakeland Africa
kwenye safari ya siku 14 za ‘Mtanzania
tembelea Tanzania’ ambayo itaanza desemba 14 mwaka huu na kumalizika
desemba 27 mwaka huu.
Mtangazaji wa
kipindi hiki Antonio Nugaz ataiongoza timu yake nzima katika safari hii ya
kuvutia huku timu yote kwa ujumla ikipata huduma ya tour guide maarufu kutoka
Lakeland Africa mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 3o katika sekta ya utalii.
Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan,
Pangani, Lushoto, Tarangire, Olduvai Gorge, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater,
Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere.
Watanzania watakaosafiri na Kampuni
ya Lakeland Africa katika safari hii ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’
watapata huduma safi ndani ya lori la kitalii wakiwa safarini ikiwemo kila
mtalii kuwa na soketi yake ya kuchajia simu, laptop na kamera.
Pia kila mtalii atakuwa na
kabati lake dogo (locker) kwa ajili ya kufungia vitu vyake vya thamani kama
vile passport, vitambulisho na kwamba kila mtalii anatakiwa kuja na kufuli lake
la kufungia kabati lake.
Mbali na hayo kila mtalii
atakuwa na taa yake ya kusomea wakati wa usiku, gari lina tanki la maji lenye
ujazo wa lita 500 na kila mtalii atapewa lita 20 kwa siku na kwamba kutakuwa na
firiji ya vinywani baridi na vitu vinavyoharibika.
Kwa mawasiliano na Lakeland
Africa
+255222-761811
+255784885901
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi
yako’
No comments:
Post a Comment