Bendi za Musiki wa
Dansi zenye miondoko ya Ndombolo ya Solo, za Twanga Pepeta na Diamond Musica
usiku wa kumkia leo zilifunika na kukonga nyoyo za wapenzi wa Muziki wa Dansi
mjini Moshi wakati wakali hao wawili walipotumbuiza katika Tamasha kubwa la
Burudani la Tusker Carnival lililofanyika katika Uwanja wa Ushirika mjini
Moshi.
Walikuwa ni Diamond Musica ndio walioanza kushambulia
Jukwaa hilo la Tusker Carnival mishale ya saa mbili usilku hadi sita kasorobo
walipo wapisha Wakongwe wa Burudani na Wabishi wa mjini Twanga Pepeta ambao
walitikisa vilivyo Mji wa Moshi.
Tamasha hilo la Tusker
Carnival lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadae kupigwa jijini
Mwanza huku Nguli wa Mziki wa dansi Koffi Antonio Olomide akiongoza
mashambulizi. Leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka
kwa Mapacha wa tatu na kundi la Extra Bongo chini ya Ali Choki.
Kijana wa Mjini Moshi ambaye anakula Maisha jijini Dar es Salaam akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha lka Tusker Carnival.
Mamaa Lwiza Mbutu akifanya makamuzi
Wacheza show wa Twanga Pepeta wakifanya makeke
Hawa ni Diamond Musica wakishambulia jukwaa la Tusker Carnival
Wadau kutoka Kampuni ya Bia ya
Serengeti tawi la Mjini Moshi nao walikuwepo ndani ya Viwanja vya Ushirika
Mjini Moshi na hapa wakishow LOVE ndani ya Tusker Carnival.
Wadau wakila Bata huku wakishushia na Tusker Baridi,
ilikuwa ni burudani na makulaji katika tamasha la Tusker Carnival.
Wadau wa Mjini Moshi nao walikuwepo uwanjani hapo.
Watu waliyarudi magoma kama kawaida
Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta akifanya vituko vyake katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika mtu nyomi zikifuatilia Burudani kutoka Tusker Carnival.
No comments:
Post a Comment