Tangazo

March 14, 2013

Benki ya Barclays kuwekeza Afrika

Benki ya Barclays inatarajia kufanya uwekezaji mkubwa katika nchi za Afrika ikiwamo Tanzania kutokana na ukuaji uchumi katika sekta mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Barclays Afrika, Kennedy Bungane, wakati viongozi wa benki hiyo walipotembelea nchini, alisema Tanzania inakua kiuchumi na kwamba gesi itakayozalishwa nchini  itaongeza ukuaji huo.

Bungane ambaye pia ni mkuu wa mikakati wa benki hiyo, alisema katika uwekezaji huo pia wataongeza huduma nyingine ili kuwafikia wananchi katika huduma za kibenki ikiwa ni kuanzisha mfumo wa mawasiliano ya kibenki kwa njia ya simu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Kihara Maina, alisema wamejipanga kikamilifu katika utoaji wa huduma za kibenki ambapo wateja watanufaika  kwa kufungua matawi zaidi.

CHANZO:Tanzania Daima

No comments: