Tangazo

March 11, 2013

Mawakala Redd’s Miss Tanzania 2013 wafundwa

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akitoa Mada kwenye Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Tanzania 2013 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wengine pichani ni Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred na Mrembo alieshika nafasi ya tatu,Eda Sylvester.

Na Mwandishi Wetu

MAWAKALA wa shindano la Redd’s Miss Tanzania kutoka maeneo kadhaa nchini, mwishoni mwa wiki walifundwa ikiwa ni ishara mpya ya kuanza kwa kinyang’anyiro hicho.
 
Katika semina maalumu kwa mawakala hao iliyofanyika Hoteli ya Giraffe iliyopo Dar es Salaam, mawakala hao wametakiwa kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria zote zinazohusu Redd’s Miss Tanzania ili kupata mrembo mwenye sifa.
 
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah, alisema ni vema kanuni na taratibu zote zikafuatwa ili kuyafanya mashindano hayo yawe na tija kwa Watanzania.
 
“Kama ninyi mkiharibu mjue kila kitu kimeharibika, hatutaki kusikia upendeleo wala aina yoyote ya ukiukwaji wa taratibu, kwetu tunataka kuona Redd’s Miss Tanzania ikifanikiwa zaidi,” alisema.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino, Hashima Lundenga naye alisema hawatasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa mawakala yoyote atakayekiuka kanuni na taratibu zilizowekwa.
 
“Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu tunataka iwe ya tofauti kuliko mika iliyopita,” alisema Lundenga. Semina hiyo pia ilihudhuriwa na watendaji kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
 
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyelitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
 
TBL kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original ndio wadhamini wakuu wa shindano la Miss Tanzania kwa sasa.

No comments: