Tangazo

October 21, 2013

BENKI YA CRDB YAKABIDHI WODI YA AKINA MAMA NA WATOTO HOSPITALI YA BUGANDO, BAADA YA KUIFANYIA UKARABATI MKUBWA


 Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimiana na baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei  akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo alipowasili katika hafla maalum ya kukabidhi wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki, baada ya kuifanyika ukarabati mkubwa na benki hiyo CRDB. Benki hiyo ilikabidhi vitanda, magodoro, mashuka pamoja na vyandarua vilivyowekwa dawa. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyadhiyay akipeana mkono na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo. (Na Mpiga Picha Wetu)  
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Mwanza, Hamis Saleh.
 Mkurugenzi wa Masoko, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akipeana mkono na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB wakiangalia uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kuzunguka eneo la Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Charles Majinge.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akiongoza zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Charles Majinge.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakimwagia maji miti ya kumbukumbu waliyopanda katika Hospitali ya Bugando. Katikati anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Godwin Semunyu.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyadhiyay akishiriki katika zoezi la kupanda miti.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) wakipaka rangi wodi ya akina mama na watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (wa tatu kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa wodi ya akina mama na watoto katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki, baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na kupatiwa msaada wa vitanda, magodoro, mashuka pamoja na vyandarua vilivyotolewa na Benki ya CRDB.
Tumezindua....
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), akizindua wodi ya akina mama na watoto kwa kufungua pazia. Kulia ni  Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Charles Majinge.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), akitandika kitanda katika wodi ya akina mama na watoto.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Bungando, Dk. Charles Majinge akipokea blanketi kutoka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wodi ya akina mama na watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Benki hiyo ilikabidhi vitanda, magodoro, vyandarua vilivyowekwa dawa pamoja na mashuka. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Saugata Bandyadhiyay. 
Picha ya pamoja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Charles Majinge.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa (kushoto), akifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Bujora kutoka jijini Mwanza kikitumbuiza katika hafla hiyo.
 Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Baadhi ya watu waliohudhuria hafla hiyo.  
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akibadilishana mawazo na maofisa wa Benki ya CRDB. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akiwaongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB kucheza kwaito. 

No comments: