Tangazo

March 8, 2014

Kampuni ya Airtel Yatoa Msaada wa Samani kwa Ofisi ya Usalama Barabarani ya Kituo cha Polisi Oysterbay

Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (wa pili kulia)akizungumza na Afisa Mnadhimu wa Polisi  Kinondoni,  SSP Bibie Juma Athumani (kushoto), baada ya Airtel kukabidhi msaada wa viti na meza kwa ajili ya Kituo cha Polisi Oysterbay hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa Polisi wa kituo hicho.

XXXXXXXXXXXXX
Dar es Salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuunga mkono serikali kupitia jeshi la polisi usalama barabarani kwa kuwapatia vifaa vya ofisi kwa ajili ya kituo cha Usalama Barabarani cha Oysterbay kilichopo wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema “Airtel inatambua umuhimu wa kazi inayofanywa na Kitengo cha Usalama Barabarani katika kusimamia na kuhakikisha usalama wa watanzania na kuamua kushirikina nao katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi. Leo tunatoa meza pamoja viti vya ofisi kwa kitu hiki cha polisi oystebay tukiamini   kwamba tutaongeza ari na moyo wa kujituma kwa maofisa hawa  na kuleta ufanisi wa kazi ,”

kwa miaka mitano mfululizo sasa Airtel imekuwa ikishirikiana na jeshi la polisi katika kufanikisha zoezi la usalama barabarani hivyo tumeonelea ni vyema kuendelea kushirikiana nao  ili kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza kazi zao  nchini.

Airtel itaendelea na dhamira yake  yakushirikiana na jeshi la polisi katika juhudi za kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa na kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa kiasi kikubwa nchini

Kwa upande wake, Afisa Mnadhimu wa Polisi  Kinondoni, SSP. Bibie Juma Athuman alisema “Naishukuru sana Airtel kwa kutoa mchango wa vifaa vya ofisi kwenye kituo changu kwani tulikuwa na uhaba mkubwa wa viti na meza za kukalia wafanyakazi pindi wakiwapo ofisini. Msaada huu utasaidia kutatua matatizo tuliyokuwa nayo na kuboresha mazingira ya wafanyakazi wa kituo hiki kuwa mazuri zaidi.  Tunawaomba makampuni mengine pia yashiriki katika kuwawezesha jeshi la polisi na kuchangia katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa kama wanavyofanya wenzetu wa Airtel.”

 Msaada huo ni muendelezo wa mpango wa Airtel kusaidia Polisi  Usalama Barabarani hapa nchini ambapo mwezi Septemba mwaka jana kampuni hiyo imetoa T-shirt zenye ujumbe Maalum wa Usalama Barabarani, stika zenye ujumbe wa kuelimisha na mafunzo kwa ajili ya kuelimisha Usalama Barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Mwanza.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Airtel Tanzania Donate furnitures to Police Office

Airtel Tanzania has continued to support the government through police force road safety by donating office equipments to  Oyster bay police station – road safety unit in Kinondoni District.

Speaking during the handover ceremony Airtel Communications and event officer Dangio Kaniki said that “Airtel recognizes the work done by the police in managing and ensuring Tanzanians safety and decided to corporate with them by improving their working environment. Today we offer office chairs and tables to oyster bay police post – road safety unit believing the aid will facilitate the police while at the office better working tools while boost their morale and efficiency.”

She further added that for the five consecutive years Airtel has partnered with the police in the road safety initiatives campaign and today we extend our support to improving their working environment to make significant strides in implementing their work in the country.

“Airtel will continue with its commitment to collaborate with police officers in an effort to ensure road safety rules are followed by citizens while road accidents are reduced significantly,” she said

For her part, The Senior Superintendent of Police Bibie Juma Athuman said “we thank Airtel for their valuable contribution; we had shortage of office furniture, this aid will enable our police to well perform their duty while in the office.  We would like to appeal to other company to join force and support us in road safety campaign and other areas as it is done by Airtel Tanzania

Airtel has been among the main sponsors of road safety and support different initiatives done to overcome the problem. Last year the company offered T – shirts with a special road safety messages, stickers and trainings to educate the entire public on the importance of following road safety.

No comments: