TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU
MUINGILIANO WA MASAFA YA EATV NA ITV KUPITIA KING’AMUZI CHA KAMPUNI YA STAR
MEDIA KATIKA KITUO CHA KUSAMBAZA MATANGAZO MAKONGO JUU
- UTANGULIZI
- Masafa ni rasilimali muhimu katika shughuli za Mawasiliano (simu, wavuti, redio, na utangazaji). Masafa ya Mawasiliano (Spectrum) hugawanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (ikitambuliwa hapa kama Mamlaka) kwa kutoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni. Moja ya kazi za Mamlaka ni pamoja na kupokea na kusuluhisha matatizo ya muingiliano wa masafa kati ya watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano kwa kutumia ujuzi na wataalamu na teknolojia ya mitambo maalumu na mahususi ya kisayansi kufanya kazi hiyo. Kazi hizi zimeainishwa katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 (TCRA Act of 2003) na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act (EPOCA) ya mwaka 2010.
- Mnamo tarehe 29 Januari 2015, Mamlaka ilipokea malalamiko kuhusu ubora wa matangazo ya vituo vya ITV na EATV yanayorushwa na Kampuni ya Star Media (T) Limited ambaye ni msambaza matangazo ya dijitali. ITV na EATV wana leseni ya Maudhui (Content Service Lisence) na Star Media wana leseni ya Miundombinu ya Utangazaji (Network Facility License as a signal distributor) kutoka TCRA. Leseni zote za Mamlaka zina masharti ya kuzingatia.
- Huduma za Mawasiliano hutumia bendi ya masafa tofauti (Spectrum bands). Huduma za mawasiliano ya setilaiti (satellite) hutumia bendi 3.4 mpaka 4.2 GHz, inayofahamika kama C-Band. Ifahamike kuwa masafa ya setilaiti ya kupokea matangazo (satellite downlink frequency) ya 3.644 GHz yanatumika kupokea matangazo kutoka satelaiti ya Intelsat 906 (TP 10) kwa matangazo ya vituo vya utangazaji nchini kupitia mfumo wa dijitali ambao mitambo yake iko katika kilima cha Makongo Juu area. Hata hivyo, sehemu nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, hutumia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.5 GHz. Masafa haya yanafahamika duniani kote kwa uwezo wake wa kutumika kiteknolojia kati ya mfumo wa “Fixed Satellite Services (FSS)” na IMT kama vile mwendo kazi wa intaneti bila waya (Broadband Wireless Access (BWA) transmission) ikiwemopia teknolojia ya WiMAX.
4. Kufuatia
malalamiko yaliyopokelewa na Mamlaka, TCRA iliteua timu ya wataalamu Wahandisi
wa Masafa kufanya uchunguzi ili kubaini tatizo la muingiliano wa masafa
yaliyosababisha ITV na EATV kutokuonekana vizuri katika king’amuzi cha Star
Media, kwa kutumia utaratibu na jinsi sheria zinavyoelekeza. Timu hiyo ya
wataalamu wa masafa iliwasiliana na Star Media na kutembelea eneo la Makongo Juu
kwenye mitambo yao ili kubaini aina ya muingiliano, muda wa muingiliano na
maeneo husika. Timu hiyo ilifanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu kwenye
eneo lenye mitambo ya kurusha matangazo ili kubaini muingiliano wa masafa
kupitia watoa huduma wa intarneti za mwendo kasi kupitia teknolojia ya WiMAX
katika bendi 3.4 – 3.6 GHz. Aidha timu ilifanya tathmini ya vipimo vya matumizi
ya masafa na watoa huduma katika bendi nzima ya C- ya kupokelea matangazo (downlink
frequency) kutoka 3.4 GHz hadi 4.2 GHz.
B. MATOKEO YA UCHUNGUZI NA YALIYOJITOKEZA
5.
Baada ya uchunguzi huo wa kitaalamu kwa
kutumia vifaa maalumu vya teknolojia ya sayansi ya masafa, timu ya wataalamu
walibaini kuwa muingiliano wa masafa ulikuwa unatokea kati ya saa 12 jioni hadi
saa 6 usiku. Uchunguzi katika eneo la urushaji wa matangazo na mitambo ya Star
Media ulibaini kuwa muingiliano ulikuwa katika mfumo wake wa kupokea matangazo
(satellite receiver station) iliyoko kwenye eneo (S 06◦ 45’ 736 E 39◦
12’ 632). Mfumo wa kupokea (Low Noise Block down converter - LNB) kutoka bendi
3.4 GHz to 4.2 GHz. Matokeo ya uchunguzi wa masafa ya bendi 3.644 GHz hayakuonesha
aina yeyote ya muingiliano. Aidha masafa ya 3.4 GHz hadi 3.6 GHz yalionesha
matumizi mbalimbali kutoka masafa ya bendi 3.5 GHz ambayo yanatumika na watoa
huduma wanaotumia teknolojia ya WiMAX.
6.
Kutokana na matokeo ya uchunguzi kama
ilivyoelezwa katika no 5, ilibainika wazi kuwa hakukuwa na muingiliano katika
bendi hiyo (In-band interference) kutoka katika mfumo wa matumizi ya inteneti
ya mwendo kasi kwani masafa yote katika mifumo yote ya utoaji huduma
haikuonesha muingiliano. Vile vile ilithibitika wazi kuwa hakukuwa na
muingiliano katika mfumo huo (out-of-band emissions) Mfumo wa huduma wa mwendo
kasi wa inteneti unaotumia masafa ya bendi 3.5 GHz huweza kusababisha
muingiliano kwa mtoa huduma anayetumia bendi 3.6 – 4.2 GHz (FSS stations).
7.
Matokeo ya vipimo vilionesha kuwa eneo la
Makongo Juu hupokea mawimbi ya Mawasiliano kutoka kwa watoa huduma wote
wanaotumia masafa ya 3.5 GHz kutoka meneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam
kutokana na eneo la Makongo kuwa juu. Hali hii inaweza kusababisha mawimbi ya
mwendo kasi wa intaneti katika masafa 3.5 GHz kuibebesha mzigo mkubwa mtambo wa kupokea matangazo ya utangazaji
(FSS stations) anayetumia bendi 3.4 – 4.2 GHz kama hakuna wigo wa kuzuia
muingiliano kiteknolojia (band pass filter) au mfumo bendi mwembamba (narrow band
LNBs).
C. KUTATULIWA KWA MUINGILIANO WA MASAFA
8. Kutokana
na vielelezo vya matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa masafa kwa
kutumia vifaa maalumu, Mamlaka ilitoa maelekezo kwa Star Media ili kutatua
tatizo la muingiliano uliokuwepo katika mtambo wake wa urushaji matangazo
Makongo Juu. Kwanza, kutumia kifaa
kiitwacho IF attenuator/filter katika mitambo yake ya kupokelea mawasiliano ya
matangazo ya setilaiti (FSS receiving station); Kutumia LNB converter katika
bendi ya masafa 3.7 – 4.2 GHz badala ya kutumia masafa ya (C-band) yote (3.4 –
4.2 GHz); hata hivyo, masafa 3.664 GHz yamehifadhiwa kama wigo unaozuia
matumizi kati ya watumiaji wa matangazo ya mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi (Terrestrial)
- (3.4-3.6 GHz) na yale ya wanaotumia Satelaiti ya kupokelea matangazo (3.7-4.2
GHz). Pili, Mamlaka ingeagiza watoaji
wa inteneti ya mwendo kasi katika mitambo yao (BWA) kuwa na nafasi ya kutosha
kati ya mitambo ya “FSS” na kufuata utaratibu uliowekwa kulingana na matumizi
ya masafa, ikizingatiwa kwamba mawimbi yaliyo mengi katika eneo la Makongo Juu
hupokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka Jiji la Dar es salaam. Tatu, njia mbadala zitumike katika
kupokea matangazo ya utangazaji katika kilima cha Makongo Juu kama vile
teknolojia ya Mkongo wa Mawasiliano (fiber
optic) satelaiti kutumia mfumo wa bendi ya Ku-Satellite band, au “microwave
links”.
9. Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kufanya
uchunguzi wa kitaalamu kwa kutumia vifaa maalumu vya sayansi na teknolojia
mahususi kwa matatizo ya muingiliano wa masafa, imebainika pasina shaka kuwa hakukuwa na hujuma yeyote kutoka kwa
Kampuni ya Star Media au kufanya kwa makusudi kwa nia ya kuharibu muonekana wa vituo husika vya ITV na
EATV katika ving’amuzi vyake. Tatizo lilikuwa ni la kisayansi na kiteknolojia
ambalo hutokea mara nyingi katika huduma za Mawasiliano kote duniani, na tatizo
hilo limemalizika kwa kutumia njia za kisayansi na kiteknolojia kwa watoa
huduma wote kwa kushirikiana na Mamlaka..
10. Mamlaka
ya Mawasiliano (TCRA) inapenda kutumia fursa hii kuwakumbusha watoa huduma wote
wenye leseni za Mamlaka kuwa inapotokea matatizo au malalamiko, basi wafuate
taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni pamoja na
kanuni zake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa TCRA na kutoa ushirikiano katika
kutatua tatizo husika kupitia sayansi na teknolojia ambayo hutumika katika
kutoa huduma za mawasiliano.
Kwa taarifa zaidi tafadhali
wasiliana nasi kupitia dg@tcra.go.tz
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
5th February 2015
No comments:
Post a Comment