Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu
cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo
itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
•
Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM
Dodoma,
Kutokana
na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini
na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa
Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti
yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu
UNI
WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata
huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na kukidhi
mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa
huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua
Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya
wanafunzi na pia tumeongeza mnara wa pili wa simu ambao
tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi wa nchi
yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya "
Tunafuraha
kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni kwani
spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari
mbalimbali za taaluma au kijamii kupitia mtandao wetu wa Airtel
"
Meneja
Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa
inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa UDOM, kwa kutumia simu zao za
mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali
mtandao wa simu wanaoutumia.
Wanaweza
kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana masaa 24 , kwa kifurushi cha
siku , wiki, mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
Fikiria!
Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi 500 tu! Alisisitiza Bi,
Muga.
Kwa
upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw,
Dick Manongi alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania
kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina
hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea
wanafunzi urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa
nchini na hata nje ya nchi ".
Ningependa
kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao
kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.
Uzinduzi
wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel
Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT)
jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.
No comments:
Post a Comment