Nalimi Mayunga
akiimba katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
- Aenda kupata mafunzo pamoja na kurekodi wimbo na video na mwanamuziki nguli Akon
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
- Aenda kupata mafunzo pamoja na kurekodi wimbo na video na mwanamuziki nguli Akon
DAR ES SALAAM
MSHINDI wa shindano la musiki la Airtel Trace Music Stars Afrika Nalimi Mayunga anatarajiwa kuondoka nchini jumatatu ya tarehe 16 Novemba kwenda Marekani kwaajili ya mafunzo na kurekodi single yake na mwanamuziki Nguli Akon.
Malimi Mayunga aliibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Afrika katika mashindano yaliyoshirikisha nchi 13 barani Afrika yaliyofanyika nchini Kenya mwanzoni mwa mwaka huu na kujishindia zawadi nono ikiwemo deal ya kurekodi wimbo na video pamoja na kupata mafunzo ya mzIki kutoka kwa mwana muziki Akon nchini marekani.
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa Airtel Bwana Jane Matinde alisema" Tunajisikia furaha kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata fulsa na kufikia ndoto zao kupitia program zetu mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Trace Music Stars, tunajivumia kumuwezesha Mayunga na kumpatai fulsa ya kujinoa kimuziki lakini pia kutanganza nchi yetu na muziki wetu ulimwenguni.
Ni matumaini yetu
kuwa , program hii itamuwezesha mayunga na vijana wengine watakao pata
nafasi ya kushiriki kubadilisha maisha yao na kuwa wanamuziki bora ndani
na nje ya nchi na kuweza kutumia vipaji vyao kama mtaji katika kuendesha
maisha yao na famila zao kwa ujumla.
Kwa upande wake Nalimi Mayunga aliwashukuru
Airtel kwa kumpatia nafasi hii ya pekee na kuhaidi kutumia fulsa hii
vyema "kwangu huu ni muujiza wa pekee kupata nafasi ya kurekodi
wimbo na kupata mafunzo toka kwa Akon, nawashukuru sana Airtel kwani mimi
binafsi nisingeweza kuonana na Akon lakini kwa kupitia program hii na ushindi
nilioupata sasa naondoka kwenda kunolewa na kupata ujuzi toka kwa Akon.
Natoa wito kwa
vijana wenzangu kutokata tamaa katika kufikia ndoto zao na
kushirikia katika mashindano kama haya pindi yanapotangazwa kwani nao
wanaweza kupata nafasi kama mimi leo.
Nimejiandaa vyema
kuwakilisha nchi yangu na kurekodi single yangu na Akon hivyo naomba
watanzania waendelee kuniunga mkono ili niweze kuwa mwanamuziki nyota
duniani.
Kufuatia ushindi huo Airtel na Trace imesamwezesha mayunga kurekodi single yake nchi South Afrika ijulikanayo kama " nice couple" nyimbo hii inapatikana youtube na pia inapigwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
No comments:
Post a Comment