Tangazo

July 11, 2016

MATUMIZI YA TIKETI ZA KAWAIDA KATIKA MABASI YA UDART MWISHO JULAI 30 MWAKA HUU

 Mabasi ya Shirika  la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART) yakiwa makao makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), David Mgwassa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari.
 Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Meneja wa Uhusiano wa Udart, Deus Bugaywa (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kaunzia Julai 30 mwaka huu kuwa ni mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa abiria badala yake zitatumika kadi.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi.

" Tiketi zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwassa.

Alisema Udart imepunguza bei ya kadi hizo kutoka sh.4500 ya awali hadi kufikia sh.2000 ili kutoa fursa kwa kila mwananchi wa kuweza kuipata kadi hizo na kuzitumia.

Mgwassa alisema kadi ziliuzwa ni 55,000 na zilizobaki ni 150,000.

Mkuu wa idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari alisema wateja wataweza kulipia kadi hizo kupitia kwa mawakala wao waliopo katika vituo vyote vya udart na kwa njia ya mitandao yote ya simu. 

No comments: