Tangazo

July 11, 2016

SOKWE MTU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE MKOANI KIGOMA YAWAVUTIA WANAHABARI

Kundi la Wanahabari wakiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (mwenye fimbo)wakijiandaa kueleke katika maeneo wanako patikana Sokwe mtu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.
Safari ya kuwatafuta Sokwe Mtu ndani ya Hifadh ya Taifa ya Milima ya Mahale ikaanza kwa kupita ndani ya msitu mnene ,mabonde na hata vipando .
Kundi la Wanahabari likiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Pascal Shelutete wakiwa wamevalia "Mask" kwa ajili ya kuzuia magonjwa yanayoweza kuambukiza kati ya Sokwe na Binadamu.
Sokwe mtu aliyepewa jina la Michio ndiye alikuwa wa kwanza kuonekana mbele ya kundi la wanahabri waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale iliyopo mkoani Kigoma.
Safari ya kuwatafuta Sokwe mtu inaendana na msemo unaosema "Huwezi kumuona Sokwe bila kutoka jasho"ili kuhamsisha wageni kuendelea kua na nguvu ya kumuona Sokwe wakati mwingine waongoza Wageni walilazimika kuelezea vitu mbalimbali vilivyoko katika hifadhi hiyo .
Wakati mwingine wageni walipata mahala kwa ajili ya kupumzika huku wakisikiliza milio ya Sokwe wapi inatokea.
Safari iliendelea.
Mwisho wa siku familia moja ya Sokwe ikaonekana ikiwa na mtoto mmoja.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kigoma.

No comments: