Tangazo

September 12, 2011

MATUKIO YA AJALI YA MELI ZANZIBAR KATIKA PICHA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Ramadhan Haji, mkazi wa Saateni Mjini Unguja, majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja, Nasra Muhsin,wa Ole Pemba akiwa amelazwa katika hopitali ya Kivunge kaskazini Unguja.Picha na Ramadhan Othman IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akifutana na Msaidizi Mkuu wa Kituo cha Afya Kivunge, Tamim Hamadi, baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU
Askari wa  vikosi vya ulinzi wakiwa katika doria kuhakikisha usalama unapatikana kwa raia  wakati wa upokeaji wa majeruhi waliokolewa katika meli iliyozama ya Mv  Spice Islander,ikitokea Unguja kuelekea Pemba.Picha na Ramadhan Othman IKULU
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akishauriana jambo na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Hospitali ya Kivunge.Picha na Ramadhan Othman IKULU
Askari wa vikosi mbalimbali vya ulinzi wakibeba  majeruhi waliookolewa katika meli iliyozama huko katika Bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja, wakifikishwa katika ufukwe wa Nungwi.Picha na Ramadhan Othman IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika eneo hilo la Ufukwe wa   Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: