Tangazo

March 7, 2012

Mkuu wa Mkoa Singida awahamasisha wananchi kujiunga Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF)

MKUU WAMKOA WA SINGIDA DR. PARSEKO KONE (ALIYESIMAMA), AMEWATAKA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA SIKU YA WADAU WA NHIF NA CHF,LILILOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA SINGIDA TRAINING CENTER,KUTUMIA FURSA HUSIKA KUIBUA CHANGAMOTO NA MAONI YENYE KULETA TIJA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU MKOANI SINGIDA SANJARI NA UHAMASISHAJI WA WANANCHI KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII NA NHIF.

KUSHOTO PICHANI NI MKUU WA WILAYA YA IRAMBA MHE.GRACE MESHACK AMBAYE  NI MWENYEKITI WA KONGAMANO LA WADAU WA NHIF NA CHF WA MKOA WA SINGIDA AKIKUSANYA MAONI YA WADAU,PIA WILAYA YAKE NI YA MFANO KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA MATIBABU KWA HOSPITAL,ZAHANATI NA  VITUO VYA AFYA NA PIA KUANDIKISHA WANANCHAMA WENGI WA MIFUKO YA AFYA YA JAMII NDANI NA NJE YA MKOA WA SINGIDA,KUSHOTO NI BWN. ALEX P. MAGESA MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA NHIF.

… UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI MUHIMU KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA  ZA MATIBABU …YAMESEMWA PICHANI NA MBUNGE WA MANYONI MAGHARIBI MHE.JOHN LWANJI AKIWA MSHIRIKI MCHANGIAJI WA KONGAMANO LA SIKU MOJA LA WADAU WA NHIF NA CHF MKOANI SINGIDA.

MTOA MADA AMBAYE NI AFISA ANAYESHUGHULIKA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII KANDA YA KATI BWN. ISAYA SHEKIFU AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MFUKO HUO KWA WADAU WAKE MKOANI SINGIDA KWENYE UKUMBI WA SINGIDA TRAINING CENTER.

MIONGONI MWA WASHIRIKI   WA KONGAMANO AKICHANGIA

No comments: