Tangazo

March 7, 2013

Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani atembelea Banda la Tanzania katika Maonyesho ya ITB

Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la nchi ya Ujerumani  akipokea zawadi ya picha yenye vinyago kutoka kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Taarishi mara baara ya kufanya naye mazungumza wakati waziri huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya dunia ya Utalii ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin jijini Berlin nchini Ujerumani Bodi ya Utalii Tanzania TTB inaongoza ujumbe wa makampuni zaidi ya 43 ya utalii  yanayoshiriki katika maonyesho hayo leo.

Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi wakati alipofanya mazungumza naye katika banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya ITB yanayoendelea jijini Berlin Ujerumani.

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Tarishi kushoto akizungumza na Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani wakati alipotembelea banda la Tanzania kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki na wa pili ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani  Christopher Mvula

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi akiagana na Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani baada ya kfanya naye mazungumzo katika banda la Tanzania 7Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi akizungumza na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani  Christopher Mvula

Veronica Ufunguo Meneja wa Huduma za Utalii Mamlaka ya Ngorongoro akizungumza na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania 9Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours Bi Zainab Ansell akizungumza na wageni waliotembelea katika banda la Kampuni yake kwenye maonyesho ya utalii ya ITB Berlin leo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours Bi Zainab Ansell akizungumza na wageni waliotembelea katika banda la Kampuni yake kwenye maonyesho ya utalii ya ITB Berlin leo.


Mwenyekiti wa Kampuni ya Langilangi Beach ya Zanzibar Tanzania Bw. Abubaker Al Amry akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake waliotembelea banda lake kwa nia ya mazungumzo ya biashara ya utalii Kulia ni Brice Guillet wa Kampuni ya Travel Technology na katikati ni Isabelle Le Bonnec wa kampuni hiyo pia.


Kazi inaendelea.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Langilangi Beach ya Zanzibar Tanzania Bw. Abubaker Al Amry kulia  akiwa katika mazungumza ya kibiashara na baadhi ya wageni katika maonyesho hayo.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki  (kushoto), akimpokea  na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula.

Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akisalimiana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani  Christopher Mvula.

Rose Abdallah Mkurugenzi wa Antelope Safaris Limited akizungumza na wageni wake waliomtembelea katika banda  la Tanzania.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali serikali zinazofanya kazi ya  utalii nchini Tanzania  wakiwa katika maonyesho hayo tayari kwa kazi ya kupokea na kutoa maelezo kwa wageni mbalimbali wanaotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya ITB yanayofanyika Jengo la Mense Berlin nchini Ujerumani. PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG

No comments: