November 30, 2012
MKUTANO MKUU WA NAMANGA SPORTS CLUB KUFANYIKA DESEMBA 09 NDEGE BEACH
![]() |
| Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu, kilichofanyika Leecar's Pub Namanga jijini Dar es Salaam. PICHA/JOHN BADI |
- KONYAGI yaupiga 'Jeki'
Na John Badi
Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu ya Namanga Sports unatarajiwa kufanyika Desemba 09, mwaka huu katika Ukumbi wa Ndege Beach uliopo katika eneo la Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi, Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Bw. David Mwaka alisema tayari makampuni kadhaa yameshajitokeza kudhamini mkutano huo.
Bw. Mwaka aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Tanzania Distilleries Ltd watengenezaji wa kinywaji maarufu cha Konyagi, Mike Commercial, Esoshi General Trading Co. Ltd na Mele DJ Co. Ltd ya Dodoma.
"Tunawashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha onyesha moyo wa kutusaidia, lakini pia tunawaomba wadhamini wengine wajitokeze zaidi ili tuweze kufanikisha mkutano wetu", alisema Bw. Mwaka.
Aidha Bw. Mwaka alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo ambao bado hawajatoa michango yao ya 20,000/- kuiwasilisha mara moja kwa watu waliopewa majukumu ya kukusanya ambao ni John Gako, Bebee Mangi na Chale JJ.
Wadau wa Takwimu wakutana jijini Dar
| Sehemu ya washiriki wa kongamano hilo. |
| Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Thomas Danielewitz akitoa hotuba yake. |
| Naibu wa Wizara ya Fedha, Dk. Saada M. Salum akifungua kongamano hilo. |
| Sehemu ya washiriki wa kongamano hilo. |
SIKU YA UKIMWI DUNIANI : WAKAZI WA JIJI LA DAR WAASWA KUPIMA AFYA ZAO NA KUJIKINGA NA UGONJWA WA UKIMWI
NAFASI ZA KAZI LEO NOVEMBA 30.2012
African Barrick Gold
DEADLINE : Dec 6, 2012, 12:57:00 PM
Gold Plant Engineering Superintendent
African Barrick Gold
DEADLINE : Dec 14, 2012, 11:12:00 AM
Alimak Superintendent
African Barrick Gold
DEADLINE : Dec 6, 2012, 10:03:00 AM
CCTV Security Coordinator
African Barrick Gold
DEADLINE : Dec 5, 2012, 5:59:00 PM
Program Officers (2 posts)
The Benjamin William Mkapa HIV/AIDSFoundation (BMAF)
DEADLINE: Friday 14th December 2012
Construction Management Officer
The Benjamin William Mkapa HIV/AIDSFoundation (BMAF)
DEADLINE: Friday 14th December 2012
Public Health Specialist (Laboratory/Molecular Biologist)
US Embassy
DEADLINE: December 12, 2012
Electrician
US Embassy
DEADLINE: December 12, 2012
Reservation and Ticketing Sales Agent
Precision Air
DEADLINE : 5th December 2012.
General Manager (1 POST)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Hr Manager(1 POST)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Finance Manager(1 POST)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Operations Manager (1 POST)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Branch Manager(3 POSTS)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Civil/Mechanical Draughtsman(2 POSTS)
Enrich Africa
DEADLINE : 15-12-2012
Fresher Marketing Graduates(15 Posts)
Enrich Africa
DEADLINE : 30-11-2012
Kwa matangazo ya kazi moja kwa moja kwenye account yako ya facebook like facebook yetu kwa ku-click HAPA
Mfumo bora wa ufuatialiaji na utoaji wa fedha utatoa motisha kwa uhifadhi na usimamizi endelevu katika sekta ya misitu kwa nchi maskini
Doha
Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji ya kupunguza hewa ukaa na uharibifu wa misitu (MKUHUMI) ulenge kunufaisha wananchi na nchi katika maeneo husika
Tanzania imesema kuwa, mfumo wa utoaji fedha kwa ajili ya kupunguza utoaji wa gesijoto na uharibifu katika sekta ya misitu hususan kwa nchi zinazoendelea unatakiwa uwe wenye manufaa kwa nchi na wananchi katika maeneo husika.
Hayo yameelezwa leo na Bwana Freddy K. Manyika, Afisa Misitu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, katika majadiliano kuhusu Mfumo wa Ufuatialia na Utaratibu wa utoaji wa fedha, yanayoendelea katika mkutano wa 18 wa nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchia unaofanyika mjini Doha, Qatar.
Akiwasilisha msimamo huo wa Tanzania, bw. Manyika ameleeza kuwa,Kuwepo kwa mfumo bora na wa ufuatialiaji na utoaji wa fedha utatoa motisha kwa uhifadhi na usimamizi endelevu katika sekta ya misitu kwa nchi maskini..
Akizungumza kwa niaba ya nchi zinazoendela (Least developed Countries -LDCs) Bw. Manyika alisema kuwa maisha ya wananchi katika nchi zinazoendelea husuan nchi maskini yanategemea sekta ya misitu kwa ajili ya kupata nishati, chakula, madawa, ujenzi wa makaazi na miundombinu, malisho ya mifugo, shughuli za kitamaduni, utalii, na huduma mbalimbali za kijamii kwa kiwango kikubwa, hivyo kwa kuzingatia umuhimu huo, mfumo wa ufuatilaiji na utaratibu wa malipo unaoandaliwa kwa ajili ya kusaidia sekta ya misitu hauna budi kutoa malipo yenye manufaa na motisha kwa wananchi wanaotunza misitu badala ya kutaka kutoa mwanya kwa makampuni ya kibiashara yenye mitaji mikubwa kunufaika na rasilimali hiyo.
“Tanzania na nchi zinazoendelea hazikubaliani na mfumo unaolenga kuwafanya wananchi wanaozungukwa na kutunza misitu hiyo kwa miaka mingi kugeuzwa vibarua na wapakazi katika makampuni yenye lengo la kujinufaisha kwa kutumia rasilimali na nguvu za wananchi maskini, Alisisitiza.”
Aidha Bw. Manyika aliongeza kuwa, kufikiwa kwa makubaliano kuhusu mfumo na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za MKUHUMI katika mkutano wa Doha utasaidia kurejesha motisha kwa wananchi kuhifadhi misitu katika maeneo yao na hivyo kuendeleza shughuli za utunzaji mazingira na kuchochea maendeleo na uhifadhi endelevu kupitia sekta ya misitu.
Katika majadiliano yanayoendelea hapa mjini Doha, nchi wanachama wanatakiwa kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa shughuli za upunguzaji wa gesijoto na utunzaji wa misitu ili kupunguza uharibifu. Mkutano wa 18 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unafanyika Doha, Qatar, kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 7 Desemba 2012.
BOB CHORA AMNG'ARISHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'
Watu wa Marekani washirikiana na Watanzania katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI
Tarehe 1 Disemba ya kila mwaka, jumuiya ya kimataifa huadhimisha siku ya UKIMWI duniani. Hii ni siku ya kutafakari kuhusu maisha yaliyopotea, na maisha yaliyobadilika milele kutokana na UKIMWI. Siku hii inatupa fursa ya kuwakumbuka zaidi ya watu milioni 34 wanaoishi na VVU duniani kote. Hali kadhalika, leo tunaadhimisha maisha yaliyookolewa na kuboreshwa nchini Tanzania na kukazia dhamira yetu ya kupambana na UKIMWI.
Aidha, tunatambua maendeleo makubwa yaliyofikiwa duniani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita kutokana na tafiti mbalimbali na mbinu za kisayansi zinazotumika katika mapambano haya. Tarehe 23 Julai 2012, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi. Clinton alitangaza kuwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) utaandaa mpango utakaoainisha awamu ijayo ya ushiriki wa Marekani katika jitihada za kimataifa za kukabiliana na UKIMWI. "Kwa upande wetu, mpango wa PEPFAR utaendelea kuwa kitovu cha utekelezaji wa azma yetu ya dhati ya kuona kuwa tunakuwa na kizazi kisicho na UKIMWI … Tungependa bunge letu lijalo la Congress, Waziri wetu wa Mambo ya Nje ajaye na wabia wetu wote wa hapa nyumbani na kote duniani wapate picha ya mambo yote tuliyojifunza na mpango utakaoonyesha mchango wetu katika kufikia azma ya kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI,” alisema Bibi Clinton.
Mojawapo kati ya mambo tuliyojifunza ni kwamba sote tuna wajibu wa kushughulikia masuala ya kimataifa yanayohusu afya na kwamba hakuna nchi yoyote inayoweza kupambana na UKIMWI peke yake. Ili kufanikiwa katika mapambano hayo ni muhimu kwa nchi kufanya kazi na wabia kama vile PEPFAR na mashirika ya kimataifa kama Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund). Kwa pamoja PEPFAR na Global Fund ziliwasaidia zaidi ya asilimia 70 ya watu wote walio katika matibabu ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI katika nchi zinazoendelea katika mwaka 2011.
Hapa Tanzania, ni lazima tuendelee kushirikiana katika kuongeza jitihada zetu dhidi ya VVU na UKIMWI. Kila mmoja wetu -- viongozi wa serikali, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidini -- ana wajibu katika jitihada hizi. Hatua ya kuiwezesha nchi yenyewe kuchukua uongozi wa programu za kukabiliana na VVU/UKIMWI ni muhimu sana katika kuhakikisha uendelevu wa programu hizo.
Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI na Marekani ikiwa na fahari kubwa kusaidia jitihada hizo. Hivi sasa Marekani, kwa kupitia PEPFAR inatoa msaada wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwa zaidi ya watu 364,000 - wanaume, wanawake na watoto.
Mafanikio haya yanayodhihirishwa na maisha ya mamilioni ya watu yaliyookolewa ni makubwa, hata hivyo bado kuna kazi kubwa mbele yetu. Tunatumia maendeleo ya sayansi ili kuhakikisha kuwa tunatumia rasilimali tulizonazo kwa ufanisi na tija zaidi ili tuweze kupata matokeo makubwa zaidi na hivyo kuokoa maisha ya watu wengi zaidi. Mathalan, tafiti zinaonyesha kuwa tohara kwa wanaume inaweza kupunguza uwezekano wa maambukizi ya VVU kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 60.
Tunapoangalia mbele, Marekani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania na wabia wake ili kuwa na mipango na shughuli za muda mrefu za kukabiliana na janga hili zitakazookoa maisha ya watu wengi zaidi. Katika kuadhimisha siku hii ya UKIMWI duniani, watu wa Marekani wanathibitisha tena dhamira yao ya dhati ya kushirikiana na Watanzania katika kufikia maono ya pamoja ya kuwa na Tanzania isiyo na VVU.
______________________________________________________________________________
Alfonso E. Lenhardt ni Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
******************************************************************************************
Every year on December 1, the global community commemorates World AIDS Day. It is a day to reflect on lives lost, and lives forever changed, as a result of AIDS. It is also an opportunity to pay tribute to more than 34 million people living with HIV worldwide. Today, we celebrate those lives saved and improved in Tanzania and recommit to the fight against AIDS.
We also acknowledge the tremendous progress the world has made in the last 30 years through research and scientific innovations in this fight. On July 23, 2012 United States Secretary of State Clinton announced that the United States President's Plan For Emergency AIDS Relief (PEPFAR) would deliver a blueprint for the next phase of U.S. efforts on global AIDS “For our part, PEPFAR will remain at the center of America’s commitment to an AIDS-free generation… We want the next Congress, the next Secretary of State, and all of our partners here at home and around the world to have a clear picture of everything we’ve learned and a roadmap that shows what we will contribute to achieving an AIDS-free generation.”
One of our lessons learned is that global health is a shared responsibility and that no country can fight AIDS alone. To succeed, it is essential that countries work together with partners such as PEPFAR and multilateral organizations like the Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria. Together, PEPFAR and the Global Fund supported over 70% of all persons on antiretroviral treatment in developing countries worldwide in 2011.
Here in Tanzania, we must continue to work together to increase our efforts in the response to HIV and AIDS. Everyone -- government leadership, the private sector, multilateral organizations, civil society, and faith-based organizations -- has a role to play. Progress toward country leadership of HIV/AIDS programs is essential for gains to be sustainable in the long term. Through PEPFAR, the United States is working closely with Tanzania to build the country’s capacity to lead, implement, and eventually pay wholly for its AIDS response with funding from the Tanzanian government, civil society and the private sector. This coincides with the 2001 Abuja Declaration in which African Union countries pledged to increase government funding for health to at least 15% of the national budget. The United States is committed to our partnership with Tanzania as it moves in this direction.
Over the last 12 months, Tanzania has made good progress in the fight against AIDS, with the United States proud to play a supporting role. In Tanzania, the United States through PEPFAR is currently supporting life-saving antiretroviral treatment for over 364,000 men, women and children. In fiscal year 2012 alone, PEPFAR directly supported more than 1.2 million people in Tanzania with care and support programs, including more than 526,000 orphans and vulnerable children. Also, its efforts around prevention of mother-to-child transmission programs have allowed more than 1.1 million pregnant women to be reached with HIV testing and counseling.
This progress, evidenced by millions of lives saved, is remarkable, but there is more to do. We are using scientific advances to focus our resources as effectively and efficiently as possible and to maximize the impact of our investments and save more lives. For example, studies have shown that male circumcision can diminish acquisition of HIV for men by over 60%. Therefore PEPFAR has increased its contribution to voluntary medical male circumcision in Tanzania eight-fold over the last three years. Prevention of mother-to-child transmission is another significant area of focus, whereby PEPFAR support has succeeded in providing prophylaxis to almost 90% of pregnant women identified as HIV-positive - protecting the health of both the mother and her child.
As we look to the future, the United States will continue to work closely with Tanzania and its partners to move toward a long-term response that saves even more lives. On this World AIDS Day, the American people reaffirm our partnership with Tanzanians in our common vision to work towards a Tanzania free of HIV.
______________________________________________________________________________
Alfonso E. Lenhardt is the Ambassador of the United States of America to the United Republic of Tanzania
"KWA TANZANIA YENYE NEEMA... INAWEZEKANA..."
SEND OFF PARTY YA DORICE ALOYCE TENDEWA
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA KANU GIDEON MOI JIJINI NAIROBI
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha KANU Mhe Gideon Moi aliyemtembelea leo Novemba 29, 2012 katika hoteli ya Nairobi Serena jijini Nairobi. |
WAHU KUPAMBA UZINDUZI WA DHANA YA 'WELLNESS' JUMAPILI HII UBUNGO PLAZA
Umewahi kulisikia hili neno?
Kwa ufupi linasanifu dhana nzima ya AFYA.
Ila afya hii inaweza kuwa ya kimwili (physical), kiakili (mental), kipesa (financial), kinahusiano (relationship), kijamii (social), kikazi(occupational), kiroho (spiritual), kihisia (emotional), kimazingira (environmental) na hata ya kitabibu (medical).
Tunahitaji afya zote hizi kuwa kamili na wenye furaha (for optimal well-being).
Dhana hii ya WELLNESS itaelezewa kwa ufupi kwa nini ni muhimu kwako katika hotel wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, jumapili tarehe 2 Desemba 2012 toka saa 8 mchana hadi 1 jioni. Wataalam wenye uzoefu katika fani hii watakuelimisha kwa muda mchache.
Uzinduzi huu utasindikizwa na mwanamuziki WAHU KAGWI toka Kenya akikuambia BETTER DAY. “Whatever you are going through today, there always gonna be a better day”.
Kiingilio: 20,000/= only per head
COME ONE, COME ALL.
Tickets zitapatikana 8020 fashions Sinza, maduka yote ya Mariedo ambayo ni IPS, Benjamini Mkapa Towers na Namanga , mlimani city Shear Illusions na Milepamba shop Mwenge Bus stop.
NB: HAKUNA TIKETI ZITAKAZOUZWA MLANGONI SIKU YA JUMAPILI. Deadline Jumamosi saa 4 asubuhi. Only limited seats
NB: Get ready to step on GREEN CARPET for pictures, the carpet of HEALTH
U.S. Embassy Public Affairs Officer (PAO) meets Association of Women in Tourism Tanzania (AWOTTA) leaders
DESIGNERS LINE UP FOR TANZANIA RED RIBBON FASHION GALA 2012
Organiser of Tanzania Red ribbon Fashion Gala Ms.Khadija Mwanamboka (second from right) at the group photo with some of the designers at her Office.
Founder and Chairperson of Tanzania Mitindo House (TMH) Ms. Khadija Mwanamboka together with the Kids from the Tanzania Mitindo House Orphanage Centre.
“My Dream is to be a top designer” One of the Orphan get trained for free at Tanzania Mitindo House Office.
DESIGNERS AND MODELS – FIRST ROUND
MOROGORO POLYTEX - VITENGE
1. EVE COLLECTIONS
a)Ava
2. SALIM ALI
a) Ben
3. MARTIN KADINDA
a) Alexia
4. EDNA SILVER
a) Nadia
5. GABRIEL MOLLEL
a) Hidaya
6. SHELLINA IBRAHIM
a) Neema
7. FRANKOO DESIGNS
a) Elgiver
8. Hameed
a) Victor
9. ASIA IDARIOUS KHAMSIN
a) Jamila
TANZANIA RED RIBBON FASHION GALA 2012
FASHION SHOW – SECOND ROUND
DESIGNERS AND MODELS
1. MUSTAFA HASSANALI
a) Jamila
b) Elgiver
c) Alexia
2. Hameed Abdul
a) Ben
b) Hidaya
3.SHELLINA IBRAHIM
a) Neema
b) Jamila
4.GABRIEL MOLLEL
a) Nadya
b) Ava
5.EDNA SILVER
a) Neema
b) Ben
7.EVE COLLECTIONS
a)Ava
b) Hidaya
6. SALIM ALLY
a)Neema
b)Victor
8. MARTIN KADINDA
a) Nadia
b) Alexia
9.FRANKO DESIGNS
a)Ben
b)Victor
10.ASIA IDARIOUS KHAMSIN
a) Elgiver
b)Jamila
EAC SUMMIT NAIROBI
November 29, 2012
SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WATAALAM WA KUREKEBISHA UPEO WA MACHO KUONA
| Dk. Hussein Mwinyi |
Na Aron Msigwa –MAELEZO
Dar es salaam.
Serikali imezindua rasmi baraza la wataalam wa kurekebisha upeo wa macho kuona nchini kwa lengo la kusimamia, kudhibiti na kuratibu utoaji wa huduma bora za macho nchini litakalofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria ya Optometria Na.12 ya mwaka 2007.
Akizindua baraza hilo lenye wajumbe 12 leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa baraza hilo lina wajibu wa kuhakikisha kuwa huduma bora za macho zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia taratibu na viwango vilivyowekwa pia kuzingatia umuhimu wa macho katika mwili wa binadamu.
Amesema maisha ya kila siku ya binadamu yanategemea uono wa macho na kuongeza kuwa hali ya kutoona inasababisha maisha ya mwanadamu kuwa hatarini na wakati mwingine kupoteza nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.
"Kila mmoja wetu anafahamu umuhimu wa macho kikiwa kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu kama vilivyo viungo vingine na tusipoona kutokana na matatizo ya macho maisha yetu yanakuwa hatarini".
Amefafanua kuwa baraza hilo lina wajibu wa kuhakikisha kuwa watoa huduma na wapokea huduma wanakua na uhusiano mzuri na kulitaka baraza hilo kutoa elimu ya afya ya macho kwa wananchi juu ya namna ya kutunza macho yao kabla ya madhara kutokea.
Dkt. Mwinyi amesema licha ya Tanzania kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalam wa macho serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa huduma za macho zinawafikia wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini.
Amelitaka baraza hilo kuweka mikakati ya kukabiliana na biashara holela ya miwani isiyokidhi viwango iliyoenea hapa nchini kwa kushirikiana na Halmashauri za manispaa ili kuondoa hatari inayoweza kulikumba taifa kutokana na kutumia miwani isiyokidhi viwango.
"Hivi sasa biashara ya miwani inayouzwa na wamachinga imeenea kila mahali nchini, jambo hili ni hatari kwa afya ya macho kwa watanzania nafahamu linatokana na utandawazi uliokithiri lakini ninyi kama baraza lazima mtafute mbinu ya kukabiliana nalo" amesisitiza.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Adam Simbeye amesema kuwa baraza hilo jipya linachukua nafasi ya baraza lililozinduliwa mwaka 2009 na kudumu kwa muda wa miaka 3.
Amesema pamoja na mambo mengine baraza hilo katika kipindi cha miaka 3 limefanikiwa kujenga na kulinda maadili ya watumishi wa fani hiyo, kulinda na kudhibiti vituo vya kutolea huduna, kufanikisha zoezi la kusajili vituo vya kutolea huduma nchini na kuhamasisha utii na ufuataji wa kanuni na taratibu za taaluma.
Aidha amesema kuwa baraza linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha na kukosa ofisi maalum ya kuendesha majukumu yake, aidha amesema baraza hilo limeshindwa kusimamia suala la wafanyabisahara ndogo ndogo (wamachinga) kuuza miwani holela mitaani.
Kwa upande wake mjumbe wa baraza hilo Bw. Anamringi Macha akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake amesema kuwa uzinduzi wa baraza hilo unawapa nguvu kisheria kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha miaka 3.
Amesema watafanya kazi kwa uadilifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata huduma bora za macho kwa mujibu wa kanuni tarattibu na viwango vilivyowekwa.
"Kuzinduliwa kwa baraza hili kunatupa nguvu kisheria kusimamia, kudhibiti na kuhakikisha huduma za macho nchini zinatolewa kwa viwango na kwa kuzingatia kanuni na taratibu na hili ndilo jukumu letu kuhakikisha maisha na afya za watanzania zinakua salama" Amesema.
Wakati huo huo serikali kwa kushirikiana na shirika la UNFPA, Mfuko wa Dunia na serikali ya Uholanzi imekabidhi magari 9 ya kubebea wagonjwa na pikipiki 107 kwa ajili ya kurahisisha huduma za ukusanyaji wa taarifa za afya, kusafirisha wagonjwa na kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto katika maeneo mbalimbali nchini.
Akikabidhi magari hayo kwa wawakilishi wa hospitali zilizopewa magari na pikipiki hizo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema magari na pikipiki hizo yamegharimu fedha nyingi na kuwataka viongozi ambao maeneo yao yamepewa vifaa hivyo kuvitunza ili vidumu na kuendelea kutoa huduma husika.
" Vifaa vilivyo katika magari haya vinatakiwa kutunzwa ili visiharibike au kuibwa ni muhimu sana kukabidhiana kwa maandishi kila inapotokea watumishi wanabadilishana zamu za kutoa huduma katika magari haya" amesisitiza Dkt. Mwinyi.
Amesema magari yenye vifaa vyote yamegharimu shilingi milioni 250 kila moja na yatapelekwa kutoa huduma ya kubebea wagonjwa katika Taassisi ya Mifupa nchini (MOI), Hospitali ya KCMC ,Hospitali za wilaya ya Maswa, Hospitali ya mama Maria wa Kanisa na wilayani Longido.
Aidha amesema magari mengine yatapelekwa katika vituo vya afya wilayani Kahama na Bukombe na kuongeza kuwa baadhi ya pikipiki zilizonunuliwa tayari zimepelekwa katika halmashauri 26 nchini.
Ole Naiko wins Lifetime Achievement Award
November 28, 2012
UZINDUZI WA JENGO LA OFISI ZA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI
NAPE AONGOZA MAELFU MAZISHI YA SHARO MILIONEA, MUHEZA
| Baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva na filam Tanzania, wakiwa kwenye mazishi ya Sharo milionea. |
| Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape. |
| Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo. |
| Mzee King Majuto akitupa mchanga kaburini kumzika Sharo Milionea. |
| Ofisa Habari wa Airtel, Jackson Mbando akiwa na baadhi ya wasanii kwenye mazishi hayo. |


