Tangazo

February 24, 2012

TANZANIA YASAINI MOU YA KUPELEKA WASHTAKIWA WA UHARAMIA WA KISOMALI KATIKA JELA HUSIKA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa  na Afrika na Mazingira ( Parliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations, economic issues, conflict resolution, and climate change)   wa Uingereza Bw  Hendry Bellingham wakishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Mh Bernad Membe akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za  kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu February 23, 2012 Lancaster House, London. (PICHA NA IKULU)

VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU KWA MARA YA KWANZA TANGIA KIJENGWE MWAKA 1967

Mkuu wa Polisi Jamii  wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya  Monduli Mkoani Arusha,Issaya Doya akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa VodacomTanzania Mwamvita Makamba, wakati wa sherehe ya kakabidhi rasmi kituo hicho kilichakarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation kwa thamani ya shilingi Milioni 17,tangu kijengwe mwaka 1967.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa  kituo cha Polisi  Mto wa Mbu kilichopo  Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha  Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha   Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya  kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hiuchi. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda  ya Kaskazini.Nguvu Kamando.

Mkuu wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Arusha.(INSP)Amilton Matangi akiwaonyesha moja ya chumba cha mahabusu Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kulia na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika kukikarabati kituo hicho tangia kijengwe mwaka 1967.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, Jumla ya shilingi Milioni17.zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC).Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha  baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi ,Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba ,Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Nguvu Kamando.

February 22, 2012

BENKI YA NBC YAJITOSA KUDHAMINI GOFU LA WANAWAKE

Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo ( wa pili kushoto)  akikabidhi mfani wa hundi ya shs milioni kwa Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo kusaidia mashindano yao yanayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo katika klabu hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni maofisa wa NBC na viongozi wa kitengo hicho cha gofu.

Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (kushoto) akizungumza kabla ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Katikati ni Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo na kulia ni Katibu wa kitengo, Joyce Svarva.

Maofisa wa NBC pamoja na wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa NBC baada ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Kutoka kushoto ni, Arden Kitomari, Meneja Chapa na Matangazo, Eddie Mhina; Mshauri wa Mawasiliano na Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo.

Waziri Nagu akutana na Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa Watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania, Zhao Zhongqiu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akiongea jambo na aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Zhao Zhongqiu leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhongqiu alimtembelea waziri huyo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akisalimiana na Mwakilishi  Mkuu mpya wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Lin Zhiyong leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhiyong anachukua nafasi ya Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza  muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk.Mary Nagu akiongea na ujumbe wa wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake  jijini Dar es Salaam . Ujumbe huo uliongelea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na China.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk.Mary Nagu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Lin Zhiyong ambaye ni Mwalikishi mpya na kulia  ni Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.

Polisi wapambana na Waandamaji Songea: Risasi za Moto zatumika

Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia wakidhibiti vurugu za maandamano  mjini Songea Mkoani Ruvuma  Februari 22.12. Maandamano hayo makubwa yalifanywa na wananchi kupinga mauaji yanafanyika katika mji huo. Hadi sasa watu wanaokadiriwa 14 wameuawa kikatili na kuondolewa baadhi ya viungo vya sehemu za siri huku taarifa ambazo hazijathibitishwa zikidai vinatumika katika matambiko kwenye migodi ya Uraniamu huko Namtumbo. Watu wawili wanasadikiwa kufa katika tukio hilo. PICHA/HISANI YA MUHIDINI AMRI - SONGEA

USD 300 000… WHAT COULD YOU DO WITH THIS MUCH MONEY?

February 2012

If you had USD 300 000 what would you do … shop ‘til you drop, start a business or buy property? Perhaps pay for more education, change your family’s life, get married or fly away?  

With M-Net’s new season of Big Brother Africa offering a huge USD 300 000 prize, this is definitely a question that will face one lucky person in 2012 after they win the popular 91-day reality series!

But only time will tell who this will be.  Right now the race is on to get into the famous house and there are just days to go before the deadline for entries closes at midnight (CAT) on Monday February 27.

So if you haven’t completed your entry and are still interested in participating…get moving because time is running out and Big Brother wants to hear from you! You and your partner may be just the people that Biggie is looking for this time round.

And a reminder … this season entrants must DOUBLE-UP to compete. This means that anyone who wants to enter season 7 must partner with another person to enter as a pair!

Entry is open to citizens from Angola, Botswana, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.  Both partners must come from the same country, must be 21 years or older, must be fluent in English and must have a valid passport.

Interested persons can collect an entry form from the nearest MultiChoice office in their country. You can also enter by visiting www.mnetafrica.com/bigbrother and completing an entry form online. Or download an entry form from the website, complete and email it back to bba@endemol.co.za.

“We’ve had positive feedback from BBA fans who love the challenge of entering in pairs,” says M-Net Africa MD Biola Alabi. “It’s great to see them embrace the change so enthusiastically! And if you haven’t sent your entry in yet, please do so soon. We want to hear from you!”

She also confirmed that, once all the entries were in, the Endemol production team will identify the best entrants and these persons will be invited to a casting session.   But if, for some reason, you don’t submit your paper entry in time…there is another option.

“We know that sometimes people do miss the cut-off for sending in their paper entry, so we’re opening the casting sessions again this year to late entries. Those people need to simply come to the casting venue and meet the team. However, a paper entry is still the very best way to get selected. It gives our teams more time to work through to your entry in detail and increases your chances of participating.”

Casting details: Holiday Inn City Centre- Dar es Salaam from 13th-15th March 2012. M-Net’s Big Brother Africa 7 starts on DStv channel 198 on Sunday May 6.

ADOLESCENT SCHOOL GIRLS TO BENEFIT FROM TZS 640 MILLION PROJECT

The Japanese Funds-in-Trust has agreed to release to The United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization-UNESCO funds amounting to US $400,000 which is equivalent to TZS 640,000,000 in order to support the Government of the United Republic of Tanzania in the implementation of a project targeting the PROVISION OF ALTERNATIVE LEARNING OPPORTUNITIES FOR ADOLESCENT GIRLS FORCED OUT OF SCHOOLS DUE TO TEENAGE PREGNANCIES.

The signing ceremony will take place at the Ministry of Education and Vocational Training conference hall at 9 AM on Thursday the 23rd of February, 2012.

The two year project will focus on out-of-school adolescent girls and young mothers between the ages of 13-19. The key project objectives are; first to provide adolescent girls who are forced to drop out of Ordinary secondary school due to pregnancies access to alternative learning opportunities and to empower them through income generating and life skills; secondly, to develop and test self-learning modules and empowerment toolkits for learners and facilitators and thirdly, to assess and document good practices and achievements which will inform strategies addressing the issues related to adolescent girls.

The overall aim of this project is improving the quality of life and social well-being of adolescent girls in Tanzania, in particular those who were forced out of Ordinary secondary school due to teenage pregnancy and truancy which is rampant in deprived rural areas. Shinyanga rural and Kahama districts will pilot the project based on the fact that Shinyanga is among the regions with a high dropout rate of adolescent girls due to early pregnancy.

It is a pre-requisite for the Plan of Operation for a Funds-in-Trust project agreement- in this case- the Japanese Funds-in-Trust (JFIT) to be signed by the Representative of the Ministry of Education and Vocational Training and the Representative of UNESCO before the funds are released.                                                              

Wateja 700 wa M-PESA wajazwa Manoti

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza
Wateja 700 wa Vodacom MPESA wamejishindia kiasi cha shilingi 35 Milioni katika wiki ya kwanza ya promosheni ya tuma fedha kwa MPESA na ushinde ilyozinduliwa wiki iliyopita ambapo jumla ya Shilingi 480 milioni kushindaniwa.

Washindi hao ambao kila mmoja amejishindia kiasi cha shilingi 50,000 katika droo za kila siku. Mbali na droo ya kila siku promosheni hiyo itachezesha droo moja kubwa kw akila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu zitakazotoa washindi wa Shilingi 10 Milioni kila mmoja.

“Hadi kufikia leo promosheni hii imeshatoa washindi mia saba, haya ni matokeo ya mwitikio mzuri wa wateja wetu kushiriki na hii inatupa faraja kwetumkwa kuwa lengo la Vodacom ni kuwafanya wateja wetu kuwa na furaha watumiapo huduma yetu ya MPESA na kuwawezesha.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza

Kupitia droo hiyo washindi mia moja hujishindia shilingi 50,000 kila mmoja ambazo mshindi huingiziwa moja kwa moja katika akunti yake ya MPESA.
.
Mwamavita amesema huduma ya MPESA imekuwa sehemu muhimu katika maisha ya wananchi ambayo imerahisha na kubadili maisha yao tangu ilipoanzishwa Aprili, 2008, na hii inaenda sambamba na azma ya Vodacom ya kuthamini mchango wa wateja wake kuunga mkono huduma hiyo kwa kuwawezesha na pia kuifanya kuzidi kuwa huduma bora,salama,ya uhakika na rahisi..
 
“Ni msimu mwengine ambapo tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufurahia huduma bora,rahisi,salama na ya kuaminika ya Vodacom MPESA kwa gharama nafuu zaidi sokoni kutoka kampuni inayoongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini. Alisema Bw. Rene katika taarifa yake kwa vyombo vya habari..

“Matumizi ya huduma ya Vodacom MPESA yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, na hii inatufanya wakati wote kuongeza kasi ya kuifanya huduma ya MPESA kuendelea kuwa huduma bora zaidi sokoni na yenye tija kwa wateja wetu inayotoa huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi. Kadri mteja anavyotuma pesa kwenda kwa mteja wa MPESA aliyesajiliwa au ambae hakusajiliwa ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya juu ya kushinda zawadi katika promosheni hii”Aliongeza Bw. Rene

Huduma ya Vodacom MPESA ina mtandao wa mawakala zaidi ya elfu kumi na tano nchi nzima na wateja zaidi ya milioni nane kati yao zaidi ya milioni mbili wakifanya miamala – kutuma na kupokea fedha kwa kipindi cha mwezi mzima mfululizo.

Kupitia huduma ya MPESA mteja wa Vodacom aliyejisajili na huduma hiyo anaweza kufanya manunuzi ama kulipia huduma mbalimbali za ikiwemo umeme – LUKU, DAWASCO,DSTV,Muda wa maongezi, kuchangia michango ya harusi,kusaidia misiba, ada, n.k ndani ya nchi na hata kutokea nje ya nchi.

Mbali na promosheni hii wateja wa MPESA kwa sasa wanafurahia pia ofa mbalimbali ikiwemo ya punguzo la asilimia 75 katika gharama za kutuma fedha kwa MPESA mabapo sas amteja anatuma fedha kwa kiwango cha chini kabisa cha shilingi 50 kuanzia shilingi 500 hadi elfu kumi, nyongeza ya bonasi ya asilimia 25 mteja anaponunua muda wa maongezi wa hewani kupitia MPESA.

Mheshimiwa 'Sugu' na Ruge sasa 'Damu Damu'

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba  wakipeana mikono  jijini Dar es Salaam Februari 21.12, ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa  tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusiana na  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu  kwa muda wa miaka miwili.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi  akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia).

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu  kwa muda wa miaka miwili.

PSPF yatoa Msaada wa Madawati katika Shule ya Msingi Bwilingu - Chalinze Pwani

Kaimu Mkurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma (PSPF), Bw. Godfrey Ngonyani (kulia) akizungumza na Wazazi na Wanafunzi pamoja na Bodi ya Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakati walipokwenda kukabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Bi. Anifa Kombo na Mjumbe wa Bodi ya PSPF Bw. Ramadhani Maneno.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Kaimu Mkurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma (PSPF), Bw. Godfrey Ngonyani (kushoto) akikabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu walioutoa leo kwa Mjumbe wa Kamati ya Shule Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani, Bi. Jacklin Kitego (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Anifa Kombo.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Baadhi ya Wanafunzi wa  Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakigombania kukaa kwenye madawati mapya 60 yenye thamani ya Milioni 3/- walioletewa na Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma PSPF.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Waziri wa Muungano Samia Suluhu atembelea ujenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akitembelea Ujenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari huko Chukwani Mjini Unguja. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayanzi ya Bahari, Dk. Margare Kyewalyanga na (kushoto) ni  Dk. Narriman Jiddawi. {Picha na Ali Meja]

Tabora Marathon 2012 kuanza Machi 1o

Mmiliki wa Orion Tabora Hotel na mdhamini wa mashindano ya Tabora Marathon 2012, Poley Ahmed (kushoto) na kulia ni Mratibu wa mashindano hayo,  Ramadhan Makula walipozungumza na waandishi wa habari. Picha na Hastin Liumba.
 ***************
CHAMA cha riadha mkoa wa Tabora (RITAM),kwa kushirikiana na Orion Tabora Hotel,wanatarajia kuendesha mashindano yatakayojulikana kama Tabora Marathon 2012 kwa lengo la kuutangaza mkoa na vivutio vyake.

Mratibu wa mashindano hayo,Ramadhan Makula,akizungumza na waandishi wa habari,katika Orion Hotel,alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji,kutangaza vivutio vilivyoko Tabora na kuaandaa vijana katika medani ya kitaifa na kimataifa.

Makula alisema wadhamni wa mashindano hayo ni Orion Tabora Hotel,chini ya usimamizi wa mkurugenzi wa hotel hiyo Poley Ahmed na mashindano hayo yanatarajia kushirikisha watu 400 wa rika mbalimbali.

Alisema licha kuasisis mashindano hayo ambayo yatakuwepo kila mwaka,Makula alisema kutakuwa na kazi za kuboresha maeneo ya kihistoria mkoani hapa ambayo ni Living stone Museum iliyopo Kwihara kata ya Itetemia manispaa Tabora.

Aliongeza maeneo hayo yataboreshwa kwa kupaka rangi hali ambayo itawawezesha wananchi na wageni mbalimbali kupata fursa ya kutembelea maeneo hayo ambayo yako kwenye historia ya nchi.

Maratibu huyo alisema wmeamua kufanya hivyo kwa kuwa wana uzalendo mkubwa na mkoa wa Tabora kwani bado mkoa haupewi kipaumbele licha ya kuwa ni mkoa wenye uiwingi wa mambo ya utalii na hata kisiasa.

Naye mdhamini mkuu wa mashindano hayo na mkurugenzi wa Orion Tabora Hotel, Poley Ahmed alisema na kutoa wito kwa vijana wa mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi kushirikia mashindano hayo ambayo yatakuwa na zawadi mbalimbali katika kilele chake.

Polet alisema licha ya yeye kuwa madhamni pia ameomba na wadau wa mchezo huo na wafadhili mbalimbali kujitokeza kufadhili mashindano hayo.

Rotary club of Dar es Salaam Launches Road Safety Campaign

In a move to lower the rate of accidents in our roads, The Rotary Club of Dar es Salaam in association with the Police force of Tanzania, is spearheading a public service campaign initiative towards driving while phoning and texting. The campaign with the theme slogan ‘Driving + Phone = Death’ is aimed and sensitizing drivers not to use their mobile phones while driving.

The President of Rotary club of Dsm Ms. Sharmila Bhatt said – the reason they launched the campaign – was to create awareness of what is slowly becoming a chronic problem and a danger to lives of other motorists not only just in Dar es Salaam but all over the country, that is phoning or texting while driving is not really worth a life. It is known that – A driver talking on a mobile is FOUR TIMES more likely to get into an accident and If you text while you drive you are EIGHT TIMES more likely to get into an accident.

The campaign is being supported by corporate companies and the Police force - who believes this sensitization, will assist in our roads being safe. 

Senior Assistant Commissioner of Police Mohamed Mpinga said –  “Phoning and texting is causing so many accidents in this country and while legislation is being worked on our utmost concern currently is having citizens driving safely and hence we joined hands with Rotary club of Dar es Salaam in this endeavour” said the commissioner adding “When a citizen is educated in the matter of safety one generally heeds rather than enforcing legislation” he said. Commissioner Mpinga urged more institutions to support the police in its efforts to make our roads safer for all users.
 
Rotary International is the world's first service club organization, with more than 1.2 million members in 33,000 clubs worldwide. Rotary club members are business leaders who work locally, regionally, and internationally to combat hunger, improve health and sanitation, provide education and job training, promote peace, and eradicate polio under the motto “Service Above Self”.

The campaign is also supported by Airtel Tanzania, Magic FM, Boss Automation Ltd, Clouds Fm and Syscorp Media

About Rotary International
Rotary International is the world's first service club organization, with more than 1.2 million members in 33,000 clubs worldwide. Rotary club members are business leaders who work locally, regionally, and internationally to combat hunger, improve health and sanitation, provide education and job training, promote peace, and eradicate polio under the motto “Service Above Self”.

February 21, 2012

NHIF WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA MKOANI TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Imanuel Humba kabla ya uzinduzi wa mradi wa kusaidia mama wajawazito na watoto wachanga ambao upo chini ya usimamizi wa NHIF kwa Mikoa ya Tanga na Mbeya kwa majaribio.  Kushoto ni Mwakilishi wa KFW, Dk Kai Gesing.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi  wa kuwasaidia kupata huduma bora kwa mama wajawazito  na watoto walio chini ya umri wa miaka 5, hususani maeneo ya vijijini.

Mmoja wa wanufaika wa mradi KfW, akipokea kitambulisho cha kupata huduma za afya kwa niaba ya wenzake 600 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi Chiku Galawa,wanaoshuhudia pemben kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NHIF, Imanuel Humba na Dr. Sweya ambaye ni Meneja wa Mradi kutoka NHIF.

Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdee akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu kuhusu namna ambavyo mradi huo unavyotekelezeka kwa kasi Mkoani Tanga kabla ya kuanza kwa mkutano wa uzinduzi.

Akina mama wajawazito waliowawakilisha wenzao 600 wakati wa kupokea vitambulisho vya huduma za afya wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafadhili wa mradi (kfW)  na NHIF.

Rais Kikwete aelekea Uingereza kwa Ziara ya Kikazi


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi. (Picha na Freddy Maro). 

Photography Exhibition: KIGOMA COLOURS


Mabondia Salehe Mkalekwa na 'Price Naseem' kutwangana Feb. 24

Bondia Salehe Mkalekwa (kushoto) na Abdalah Mohamed (Prince Nasem) wakitunishiana misuri Dar es salaam jana wakati  wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa KG 67 Watel weight litakalofanyika feb 24. Katikati ni mratibu wa mpambano huo, Shabani Adios 'Mwaya Mwaya'.Picha na superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prenc Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake
wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa

Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New
Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.

Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuinua mabondia  ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Debe watakaopigana uzito wa kg 55,
Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Dickson Kawiani na Kulwa Kindondi atakayepigana na Khaji Hamisi.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones, Lenox Lewis,David Haye na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Ngumi, Rajabu Mhamila Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

February 20, 2012

Wanaume wagoma kula majumbani mwao nchini Kenya kufuatia vipigo toka kwa Wake zao

Mwenyekiti wa chama cha wanaume,  Nderitu Njoka akimfariji baba aliyepigwa na mkewe.
****************
Wanaume nchini Kenya wanapanga kugomea vyakula vya mabibi zao kwa siku sita kutoka na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga mabwana zao.

Badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni.

Mwenyekiti wa Chama cha maendeleo ya Kina baba Nderitu Njoka amesema mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.

Kiongozi huyo Nderitu Njoka amesema kuanzia leo jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akinababa kula mahotelini badala ya majumbani mwao.

Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wauaume alikuwa akizungumza katika hospitali kuu ya mjini Nakuru huko Rift valley ambako alikuwa amekwenda kumliwaza baba mmoja ambaye amelezwa humo kutokana na kipigo alichopewa na mkewe.

Baba huyo akizungumza kwa uchungu hospitalini alisema mkewe alimuita nyumbani it akachukuwe pesa kabla ya kumfungia chumbani na kumtandika.

Kwa muujibu wa bwana Nderitu Njoka, mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopigwa na bibi zao.

Katika mkoa huo wa kati wanaume karibu nusu milioni wameripoti kutandikwa.

Chama hicho cha wanaume kimedai kuwa kuna wanaume ambao wanalazimishwa kufuo nguo za wake zao.

Wengine pia wamedai kunyimwa tendo la ngono na mabibi zao.

Jijini Nairobi wanaume ambao huona kivumbi kutoka kwa wake zao ni laki tatu.

Lakini baadhi ya akina mama kutoka mkoa huo wanasema akina baba ndio wa kulaumiwa kwa kushindwa na majukumu yao ya kifamila.

Wanasema waume wangi wamekuwa waume suruali tu.

Hata hivyo wengi wanasubiri kuona kama kweli mgomo huo utafaulu, na ni wanaume wangapi walio na pesa za kwenda kula hotelini badala ya kula majumbani mwao.
Source:BBC Swahili

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lawamani kufuatia Kifo cha Mwanachuo kilichotokea Siku ya Wapendanao 'Valentines Day'

Marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha TEKU aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao 'valentine day'.

Baadhi ya majeraha yaliyotokana na kipigo katika mwili wa marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Baadhi ya majeraha yaliyoyokana na kipigo atika mwili wa marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31).
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia mkoani MBEYA katika matukio matatu tofauti, likiwemo la tukio la Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].

Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika matembezi ambapo polisi walikuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].

Pia marehemu aliporwa shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononi .

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.

Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.

Tukio la pili marehemu Zuberi Mwajeleba (21) mkazi wa kijiji cha Ibumba wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambaye alinyongwa kisha mwili wake kutupwa katika mto wa Kanyegele wilayani humo.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Katika tukio la tatu limetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilomba jijini Mbeya ambapo pikipiki yenye namba za usajili T 834 BOX aina ya Shinray ambayo dereva wake bado hajafahika alimgonga mtoto Mildred Immanuel (10) mkazi wa eneo hilo.

Hata hivyo dereva alitoroka na kuitelekeza pikipiki katika eneo la tukio na pikipiki hiyo imehifadhiwa katika Kituo cha kati cha Jeshi la Polisi, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya na Polisi wanafanya juhudi za kumtafuta dereva huyo.

HABARI YA KUFUFUKA.
Wakati huo huo katika hali isiokuwa ya kawaida Roza Simbeye ambaye ni mama wa mtoto mmoja katika kitongoji cha Isandula, kijiji cha Vuwile, Kata ya Isandula, aliyefariki Februari 16 majira ya saa kumi na mbili za jioni amefufuka wakati taratibu zote za mazishi zipokamilika kama kuchimba kaburi na kuchonga jeneza na taratibu za ibada.

Na ilipofika majira ya saa 3:30 asubuhi ya Februari 17 baada ya kaburi kuchimbwa na jeneza kukamilika zilianza taratibu za kuchukua mwili wa marehemu Roza chumbani ndipo watu waliopewa jukumu la kumwosha walishangaa kumwona marehemu akiwa hai huku akiwa amtoa macho kama vile mtu ametoka usingizini ambapo mpaka sasa kaburi halijafukiwa wala jeneza halijatumiwa na kufanya wanakijiji kubaki na mshangao.
Habari na Picha kwa Hisani ya Mbeya Yetu Blog

Usafiri wa Wabunge kuelekea Bungeni Dodoma Mwaka 1984! kumbe inawezekana!!


Rais Dk.Jakaya Kikwete aongoza sherehe za Ugawaji mifugo kwa kaya zilizoathirika na ukame Longido

Mzee wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli.

Viongozi wa kabila la Kimasai (Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.

Mmoja wa Wazee wa Kimasai akimuombea dua Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wailayani Longido Jumapili. PICHA/FREDDY MARO
*************************************************************************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mradi Kabambe wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo (Seed Stock) wa kutoa kifuta machozi cha mifugo kwa maelfu ya wananchi katika wilaya tatu za Mkoa wa Arusha mifugo ambao walipoteza mifugo yao wakati wa ukame mkubwa ulioendelea kwa miaka mitatu mfululizo katika wilaya hizo.

Rais Kikwete amezindua Mradi huo katika sherehe kubwa iliyofanyika mjini Longido jana, Jumapili, Februari 19, 2012, ambako amekabidhi ng’ombe jike watano na mbuzi watano kwa kila moja ya kaya 2,852 zilizopoteza mifugo hasa ng’ombe katika wilaya hiyo wakati wa ukame huo mkali ambao ulifikia kilele chake kwa mwaka 2008/2009.

Kiasi cha ng’ombe majike 500 wametolewa kwa wananchi wa Wilaya ya Longido katika sherehe ya jana iliyohudhuriwa na viongozi kutoka wilaya zote tatu wakiwemo viongozi wa Serikali, viongozi wa halmashauri, wabunge, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa William Lukuvi wananchi wa Wilaya ya Longido wamemshukuru kwa dhati Mheshimiwa Kikwete na Serikali yake kwa kubuni na kutekeleza Mradi huo wa aina yake ambao haujapata kubuniwa ama kutelekezwa na Serikali yoyote tokea Uhuru.

Chini ya Mradi huo ambao utagharimu kiasi cha sh bilioni 11.2, kaya 6, 127 katika wilaya za Longido, Ngorongoro na Monduli, zote za Mkoa wa Arusha, zitapewa kifuta machozi cha ng’ombe majike watano na dume mmoja (ama mbuzi badala ya dume kama walivyoamua wananchi wa Longido), ili kuwawezesha wananchi kuanza tena kujenga misingi ya mifugo yao ambayo ilipotea katika ukame mkubwa ambao ulifikia kilele chake mwaka 2009.

Mbali na kutoa kifuta machozi cha mifugo, Serikali imekuwa inatoa misaada ya chakula cha dharura kwa wananchi wa maeneo hayo tokea wakati wa ukame huo. Wilaya ya Longido pekee yake mara nane imepokea chakula cha dharura cha kiasi cha tani 11,000 katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa kikosikazi cha Serikali kilichofanya tathmini ya upotevu wa mifugo kutokana na ukame huo, Wilaya ya Longido ilipoteza ng’ombe 231,832, mbuzi 171,435 na kondoo 92,235, Wilaya ya Ngorongoro ilipoteza ngo’mbe 115, 422 na Wilaya ya Monduli ilipoteza ngo’mbe 56,585, mbuzi 39,766 na kondoo 28,883.

Hatua ya utoaji ngo’mbe kwa wananchi wa Wilaya la Longido ambao utafuatiwa na utoaji wa ngo’ombe kwa wananchi wa wilaya za Ngongoro na Monduli, ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete alipotembelea Wilaya ya Longido Agosti 23, mwaka 2009, na kushtushwa na madhara yaliyokuwa yamesababishwa na ukame katika wilaya hiyo. Rais Kikwete alirudia ahadi yake hiyo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika mikutano yake ya kampeni mjini Longido na katika eneo la Namanga.

Kwa mujibu wa Mradi huo, jumla ya ngo’ombe 25, 055 na wastani wa mbuzi 14, 260 (watano kwa kila kaya) watatolewa na Serikali ambako Halmashauri ya Wilaya ya Monduli itapata ngo’mbe 6,184, Halmashauri ya Wilaya ya Longido ng’ombe majike 11, 408 na wastani wa mbuzi 14, 260 wakati Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro itapata ngo’mbe 7, 463.

Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ngo’mbe wanaotolewa kwa wananchi siyo fidia ya mifugo yao ambayo ilipotea wakati wa ukame bali ni kifuta machozi tu.

“Hatuna uwezo wa kuwafidia wananchi ngo’mbe wote waliopotea katika ukame ule. Lakini kama Serikali lazima tufanye jitihada za kuwawezesha wananchi wa Masai kurejea katika shughuli yao kuu yaani ufungaji kwa kutoa kifuta machozi tu kidogo. Bila ngo’mbe hakuna Mmasai.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

AIRTEL ESTABLISHES WIDEST COVERAGE RURAL IN TANZANIA

Mwanga District Council Chairman Ms. Theresia Msuya cut the ribbon to officiate the launch of Airtel communications tower at Mgagao village where the tower will provide communications services to more than four villages in the district, looking on is Semshitu Msangi Airtel Sales Officer 1st from left along with other leaders of the village at the weekend. 
**********************************************************************************
Airtel, a telecommunication Company has launched the communication tower at Mgagao village, Mwanga district in Kilimanjaro region which will help in operation of four villages around Mgagao such as Makungwini, Mambarale, Kingondi, and pangalo.

Speaking during the launch, Airtel’s Northern marketing Manager Semshitu Msangi said that ‘’Airtel as the widest coverage telecommunication in Tanzania will proceed with its policy of giving the reliable network and affordable one to the people of rural village and urban areas, we know that communication has the big role in our community such as in implementation of security, upgrading the economic level.

Our focus is to make sure that, the community are together by doing so we are making sure that the rural areas are having the reliable communication and affordable because in rural areas is where there is a lot of challenges‘.

“Now day’s people of Mgagao village and the surrounding villages have the opportunity to access all Airtel products and services such as money transfer “Airtel Money” , Internet services ,and they enjoy affordable rates while calling and sending the messages, Msangi added”

On behalf of the people of Mgagao village, Mwanga District Council Chairman Ms.Theresia Msuya said “thanks to Airtel Telecommunication Company for giving us this unique opportunity of having reliable communication network here in Mwanga district.

"Thanks Airtel for your shore up to these communities which was real facing communication challenges we had before such as absence of network at all in Mwanga district. Also I would like to urge Airtel to ensure continuity of their plans for future rollout of their network in an effort to accelerate the rural development and economic enhancement of our people. We are together, and ready to continue improving the working environment to encourage more investment within our region rural areas.

"The launching of Mgagao tower will enable the neighboring village such as Makungwini, Mambarale, Kingondi and Pangalo to have communication network from Mgagao tower. We thanks Airtel for giving us the reliable and affordable network which have the widest coverage, that everywhere you go Airtel will be with you"  Mwanga district ward Chairman Ms.Theresia Msuya added Airtel Tanzania is the mostly forehead company to make sure mobile communication is reaching all Tanzanians nationwide especially in rural village.