Tangazo

April 30, 2012

Wana CUF wamlaki Rais Jakaya Kikwete kwa shangwe baada ya kuwasili jijini Tanga leo



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya  leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi. PICHA NA IKULU

Miss Ukonga na Miss Tabata wafanya mazoezi ya pamoja

 Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati walipofanya mazoezi ya pamoja jana.


 Baadhi ya waremnbo wa Tabata wakipita kwa mwendo wa madaha.

Ngoma ya asili nayo imo na hapa ni kucheza kwenda mbele.

Mwandaaji wa Miss Tabata, Freddy Ogot (katikati) akiwaeleza jambo waandaaji wa Miss Ukonga 2012.   

Hiki nacho kipaji!


WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA KIKAO CHA SAGCOT

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao cha Investment Forum SAGCOT Local Investors, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Aprili 30, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ASKARI POLISI MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA PIKIPIKI MKOANI KIGOMA

Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma

 Askari Polisi mmoja wa Kikosi cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Kostebo Shaban Hamisi Gobeka(37), amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua akiendesha kuacha njia na kugonga mti kushoto pembeni mwa barabara ya Lumumba mjini Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishns Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 12.15 jioni katika mtelemko mkali eneo la Lubengela wakati askari huyo akiendesha pikipiki yenye namba T.757 BYY aina ya Toyo akitokea Mwanga kuelekea Kigoma mjini.

Kamanda Kashai amesema wakati wa ajali hiyo Kostebo Gobeka mwenye namba F. 1561 alikuwa amempakia kijana mwingine aitwaye Filbert Kibuka(25) mkazi wa Mwanga mjini Kigoma ambaye yeye amejeruhuwa vibaya na amelazwa katika Hospitali ya mkoa Maweni kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuwa ni mbaya.

Amesema ingawa Polisi bado inachunguza chanzo cha ajali hiyo, lakini imebainika kuwa imesababishwa na mwendo kasi uliotokana na kukatika kwa bleki ya pikipiki hiyo huku ikiwa kwenye mteremko mkali.

Kamanda Kashai amesema Konstebo Gobeka alikuwa ni dereva wa kutumainiwa wa pikipiki za Polisi na alipata mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki ambapo kabla ya kuhamishiwa kikosi cha mawasiliano ya Polisi mkoani hapo, marehemu alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa wakiendesha pikipiki za doria mkoani Kigoma na hakuwa na kumbukumbu zozote za ajali.

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema Jeshi la Polisi limempoteza Askari shupavu na mchapakazi lakini pia amesema pikipiki aliyopatanayo ajali Askari huyo haikuwa mali ya Jeshi la Polisi.

TBL YASHINDA TUZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga. (PICHA/MPIGAPICHA WETU)

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.

Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.

Serengeti Breweries Limited (SBL) announce Mr. Steve Gannon as Managing Director

Mr. Steve Gannon
Serengeti Breweries Limited (SBL) is pleased to announce the appointment of Mr. Steve Gannon as Managing Director, effective 1 July 2012. Mr.

Steve Gannon joins SBL from Diageo Cameroon Hub where he has been Managing Director since 2009.

In this role at the helm of SBL, Mr. Gannon will be a member of the East African Breweries Ltd Executive committee.
 
Under Mr. Gannon’s leadership for three years, the Diageo Cameroun Hub business has delivered significant share growth in beer and established new businesses in premium spirits.

During Mr. Steve Gannon’s tenure leading the Diageo Cameroun Hub business he has led significant investment behind building capacity and expanding the businesses routes to market.

In addition, Mr. Gannon has been central in leading the development of the Business Coalition Against Corruption in Cameroon – an unprecedented initiative in partnership with the Cameroon government to create a private sector movement united against corruption.

Prior to his role within Diageo Cameroun Hub, Mr. Steve Gannon has had 30 years commercial experience in Diageo, including leading the Diageo Venture Africa Business, launching the Guinness brand in a number of African markets as well as doubling the Diageo Africa spirits business in the Diageo Venture Africa markets.

Breaking News: Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillary avuliwa Ubunge na Mahakama

Habari zilizotufikia punde katika chumba chetu cha habari ni kuwa aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) Aeshi Hillary  (pichani) amevuliwa ubunge na mahakama, kufuati hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Sumbawanga Mjini dhidi ya Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye alidai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

    Miongoni mwa madai mengine ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki n.k.

Daily Mitikasi Blog inaendelea kufuatilia taarifa zaidi mtajulishwa punde.

Airtel yachangia Ujenzi wa Kituo cha Afya Pemba - Michenzani: Yatoa Vifaa vya Ujenzi vya Milioni 10/-

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Saruji 143 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiawani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Wakwanza kulia ni sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Kombo na kati ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Nondo 62 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiwani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

*****************
 . Kituo hicho kitafaidisha zaidi ya watu 9,000 wa maeneo ya Bogoa, Shidi na  Michenzani
   

. Airtel yakabidhidhi Mabati 264,  Saruji 143, Nondo 62 na Mbao za kupau kituo cha Afya Michenzani
 

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa huduma maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi.

Airtel Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet ya  3.75G.

Kwa upande wake Sheha wa Michenzani akipokea  msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel.

“ naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha ujenzi wa  kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein  ambae wiki moja iliopita aliweka jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza  ujenzi wa kituo hiki uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa katika kituo kimoja kile cha Bogoa.

Nae Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.

“Ninaipongeza Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia  (Serikali ya Mtaa) iwe na kituo chake cha Afya.

Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.” Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa  lengo la kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .

Mwaka huu wa 2012 pia Airtel  imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha miundombinu ya Afya  Visiwani Zanzibar.

SEA BREEZE RESIDENTIAL COMPLEX/APARTMENTS SELLING AT JANGWANI BEACH





17 Km from City Center, Old Bagamoyo Road
Located at Africana Jangwani Beach
Plot No. 192, Near White Sands
Kilongawime Yard
Kinondoni District
Dar-Es-Salaam (Tanzania)

Features
Stylish and spacious apartments with dedicated parking facilities and exquisite landscaping that will provide the ultimate peace of mind.
Pool Facing Unit Layout
96 elegant apartments are located along the middle of the complex facing the pool side Each of almost 150 square meters (or 1600 square feet)
Each unit contains:
• 1 master bedroom with its own bathroom & dedicated dressing area.
• 2 bedrooms each with its own bathroom ensuite.
• Living room and dining area
• Kitchen with attached storeroom
• Utility room
• Powder room for visitors
• 2 balconies.

Garden Facing Unit Layout:
128 spacious apartments are located facing the gardens and overlooking the central apartments. Each of almost 170 square meters (or 1800 square feet)
Each unit contains:
2 master bedrooms with their own bathrooms & dedicated dressing areas.
1 bedroom each with ensuite  bathroom.
 Living room and dining area
Kitchen with attached storeroom
Utility room
Powder room for visitors
2 balconies.
Stylish interiors
UPVC windows
Vitrified tiles
Dedicated parking space for at least one car
Access to guest parking
Common Services in the complex:
24 hours security services
24 hours backup generator
Community hall for parties and functions
Fitness facilities including a pool,
basketball court
Clubhouse
Children’s play area
On-site convenience stores

Sales
The Process
Global Land Solutions Limited (GLS) is dedicated to making the sales process as easy for you as possible. The steps below outline the process for securing your new home.
1.    Site visit to see model home and location.
2.    letter of offer(to be signed and returned within 7 days of receipt)
1.    securing choice of apartment block allocation (block #, apt #)
2.    agreement of payment plan
3.    10% deposit (partially refundable)
3.    Sales agreement – final binding document (to be signed and returned within 14 days of receipt)
4.    June 2013 – completion of payment and handing over of apartment.
Pricing
Pricing varies by when the sales agreement is signed. The table below shows the pricing structure based on the month of signing.

    USD                                                              Tshs      
Special Offer Price    $110,000       176,000,000      
April – June    $130,000                     208,000,000      
July – September    $140,000          224,000,000      
October onwards    $150,000           240,000,000   
 
Payment Options
GLS has 3 payment plans to enable you to acquire a home in this vibrant and unique community.
 
Option 1: Full Upfront Payment Plan
This is the quickest and simplest of our payment plans. It ensures that you get the best deal with minimal transaction costs.
·    100% upfront payment upon signing of letter of offer (non-refundable).
 
 Option 2 – Out of Pocket Payment Plan
This payment plan allows you until June 2013 to complete your payments with your last payment being in June 2013, at which point construction will have been completed and your new home will be ready for you to move into.
·    10% deposit required at signing letter of offer (partially refundable)


Sign Agreement    Cost of Apartment    10% Deposit    Number of Payment Months    Minimum Monthly Payment (Last payment June 2013) 
     
Apr-2012     $130,000    $13,000    14    $8,357.14      
May-2012    $130,000    $13,000    13    $9,000.00      
Jun-2012     $130,000    $13,000    12    $9,750.00      
Jul-2012      $140,000    $14,000    11    $11,454.55      
Aug-2012     $140,000    $14,000    10    $12,600.00      
Sep-2012     $140,000    $14,000    9    $14,000.00      
Oct-2012     $150,000    $15,000    8    $16,875.00      
Nov-2012    $150,000    $15,000    7    $19,285.71      
Dec-2012     $150,000    $15,000    6    $22,500.00     

Option 3 – Long Term Payment Plan:
This payment plan allows you to pay for your new home while you live in it and at your own pace. By getting a mortgage from your bank you can make smaller payments for up to 180 months. GLS will assist you by providing supporting documentation required in securing your home loan.

·    10% deposit required at signing letter of offer (partially refundable)
·    20% down payment for Mortgage facility with bank
·    Mortgages can be for up to 15 years (180 months) so payments can be even lower.
 
Sign Agreement    Cost of Apartment    10% Deposit    20% Mortgage Down payment*    Number of Months (15 year mortgage)    Estimated Monthly Mortgage Payment*      
 
Apr-June            $130,000    $13,000    $26,000    180    $1,465.48      
Jul-Sept              $140,000    $14,000    $28,000    180    $1,578.21      
Oct-Onwards    $150,000    $15,000    $30,000    180    $1,690.94     
 
* amounts to be agreed with lending institution – figures for demonstration purposes only.


VIJANA WA ELIMU YA JUU WATINGA CCM KUFIKISHA UJUMBE WAO DHIDI YA MAFISADI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea  Vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika  leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.

Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.

Vijana wakionyesha bango la kuwataka 'magamba' waendelee kujitoa CCM..

Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.

Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika  leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

Bondia Francis Cheka amgaragaza Mada Maugo

Mada Maugo (kushoto) na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi.

Cheka (kushoto) akipiga ngumi bila mafanikio uku mada akiludi nyuma kujiami.

Meya wa Manspaa ya Ilala, Jery Slaa akimvalisha mkanda bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa K.O raundi ya sita jana.

Meya wa Manspaa ya Ilala, Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa K.O raundi ya sita jana. picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MWIGULU AVALIA NJUGA BARABARA YA MAJOHE

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba akimkabidhi cheti cha umahiri wa hisabati, Agnes Myolele, wakati wa mahafali ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu daraja la IIIA, yaliyofanyika leo katika Chuo Cha Ualimu cha West Dar es Salaam, Majohe Rada, wilayani Ilala. Kulia ni Mkurugenzi wa chuo hicho Kenedy Makuza. Jumla ya wahitimu 98 walitunukiwa vyeti. (Picha na Bashir Nkoromo).

NA MWANDISHI WETU 

KATIBU wa NEC, Uchumia na Fedha Mwigulu Nchemba ameahidi kuzungumza na Mbunge wa jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Eugine Mwaiposi kuangalia uwezekano wa kuifanyia ukarabati wa barabara ya Majohe ili iweze kupitika kwa urahisi misimu yote.

Amesema kukarabatiwa kwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa tano, inaungana na barabara ya Pugu kwenda katika maeneo mbalimbali ya Majohe, kutasaidia shughuli nyingi za kijamii kufanyika kwa urahisi.

Mwigulu alisema hayo, leo wakati akizungumza kwenye mahafali ya Chuo Cha Ualimu cha West Dar es Salaam, kilichopo Majohe Rada, jimboni humo, ambapo aliwatunuku pia vyeti wahitimu 98 wa ualimu daraja la III A.

"Kwa bahati nzuri naijua, kwa kweli si nzuri kupitika hasa nyakati za mvua, nitazungumza na mbunge wa jimbo hili ili tuone uwezekano wa kuifanyia ukarabati  ikiwemo kuwekwa lami", alisema.

Alisema pamoja na kumshauri mbunge lakini wakati wa kikao cha bajeti kijacho atakuwa mstari wa mbele kuunga mkono ombi la kujengwa barabara hiyo kupitia bajeti kuu ya serikali.

Mwigulu alitoa majibu hayo kufuatia ombi lililotolewa na mkuu wa chuo hicho, Kenedy Makuza ambaye alisema wakazi wa Majohe na wanafunzi wa chuo chake wamekuwa wakipata taabu kwenda mjini kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Wakisoma risala, wahitimu waliomba utaratibu wa kuruhusu wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la VI-27 kujiunga na vyuo vya ualimu uendelee angalau kwa miaka miwili ijayo kwa kuwa ukiondolewa utaratibu huo wengi watashindwa kujinga na vyuo hivyo.

Walisema, wengi wa wanafunzi wamekuwa wakishindwa kupata daraja kubwa katika mitihani ya sekondari kutokana si kwa kkukosa akili kimasomo lakini ni kutokana na mzingira ya shule wanamosoma ambazo walisema nyingi hazina mazingira bora na vifaa vya kusomea kuwawezesha kushinda vizuri.

Katika hotoba yake, Mwigulu aliunga mkono ombi hilo na kuahindi kulipeleka kwenye vikao vya juu vya uongozi wa CCM ili liweze kutolewa maamuzi na serikali.

Pia Mwigulu ameahidi kuisaidia Chuo hicho kwa kukipatia vifaa vya michezo ikiwemo mipira.

Aliwataka wahitimu kwenda kuwa mabalozi bora katika jamii na kutumia uelewa wao kutokana na elimu waliyonayo, kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo na wa kushiriki kutoa maoni wakati wa mchakato wa kupata amaoni ya wananchi kuelekea uundwaji katiba mpya.

April 27, 2012

KAMATI KUU YA CCM YARIDHIA RAIS KUVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo,Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana leo mjini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine imeridhia Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawqaziri.
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

      Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioainishwa na  taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;


        1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao. Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

           2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais   KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoainishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

           Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
          
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Spika Makinda anataka kumtoa kafara Jairo?

Mchanganuo wa matumizi ya fedha zilizoombwa na Jairo kwenye taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kwa ajili  ya kulipa posho kwa watumishi wa wizara na taasisi hizo wakati wa kujadiliwa bajeti ya Nishati na bungeni Dodoma mwaka jana.

 
Fomu inayoonesha posho walizolipwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  na Naibu wake, Adam Malima wakati wa Kikakao cha Bunge cha kujadili bajeti ya wizara  hiyo, Dodoma mwaka jana.
WAKATI akiahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma wiki hii, hadi Juni 12 mwaka huu wakati wa kujadili Bajeti ya Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitoa kauli inayotatanisha.

Makinda alisema: "Ndugu zangu wabunge na mawaziri mliosemwa hapa bungeni, msichukie na kufika hatua ya kuumia bure mkanuniana... haya yaliyosemwa hapa ni maneno tu na yameishia hapahapa. Msiendelee kuyawaza sana wakati mwingine hata waliowasema wameshaondoka na hata hawayakumbuki."

"Yaliyojadiliwa yote ni kwa nia njema. Isiwe kiini cha chuki na uhasama. Msibebe chuki ndani ya roho zenu. Msichukue hasira mpaka mkapasuka mifupa. Mnaambiwa namna ya kufanya kazi vizuri. Mkichukulia kwamba ni uadui, mtapata shida," alisema Makinda na kusisitiza juu ya dhana nzima ya cheo ni dhamana kwa kuongeza: "Kama husemwi wamseme nani na wewe ni Waziri?"

Kauli hii ya Spika ambaye ni kiongozi mkuu wa Bunge inadhihirisha kwamba wabunge wetu ni wapiga porojo tu wawapo 'mjengoni'.

Spika akataa ripoti ya Jairo

Mantiki ya kuweka utangulizi wa kauli hiyo ya Spika Makinda katika uchambuzi wangu ni kutokana na kukataa taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Bunge juu ya tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyesimamishwa, David Jairo.

Taarifa hiyo ambayo ilikuwa iwasilishwe bungeni juzi na Serikali kwa mujibu wa ratiba, lakini haikuwasilishwa na Makinda aliliambia Bunge kuwa alilazimika kuikataa kwa madai kwamba majibu ya Serikali hayakumridhisha akidai haikidhi matakwa ya Bunge.

Ripoti hiyo ilitarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa Jumatatu, baada ya Jairo kuingia katika kashfa wizara yake ilipowasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/12 iliyoibuliwa na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, aliyedai alichangisha sh. bilioni moja kutoka kwenye taasisi zilizo chini ya wizara yake ili kusaidia kupitishwa kwa bajeti hiyo.

Baada ya wabunge kutoa madai hayo, Serikali ilichunguza suala hilo kupitia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliyebaini fedha zilizokusanywa hazikuwa kiasi hicho.

Uamuzi huo wa CAG ulitangazwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuwa Jairo hakuwa na makosa na akamwamuru arejee kazini kwa vile hakuna sehemu ambayo alivunja taratibu za kazi.

Kamati Teule

Hali hiyo iliwaudhi wabunge waliolazimika kuunda Kamati Teule ya Bunge ambayo katika uchunguzi wake ilimtia hatiani Jairo, hivyo wakataka Serikali ichukue hatua za kinidhamu juu ya mtumishi huyo wa umma.

Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza sakata la Jairo iliongozwa na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani (CCM), ilikuwa na hadidu za rejea tano zilizotakiwa kufanyiwa kazi.

Wajumbe wengine katika kamati hiyo walikuwa ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Umbula, Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) na Mbunge wa Karagwe, Godbless Blandesi.

Majibu ya Makinda yalikuja baada ya Mbunge wa Karatu, Israel Natse(Chadema) kuomba mwongozo wa Spika na kuhoji ni kwa nini suala la Jairo liliondolewa katika orodha.

Mchungaji Natse aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata la Jairo kuhusu kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwezesha kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, alionesha kukerwa na kitendo cha kuondoa kwenye orodha taarifa hiyo.

Spika Makinda alidai kuondoa ripoti hiyo ni kutokana na kutokamilika kama ilivyokusudiwa, hivyo akadai upungufu huo hauwezeshi wala haumshawishi kuruhusu itolewe mbele ya Bunge.

Kauli hiyo ya Makinda ndiyo imenipa msukumo wa kuandika uchambuzi kuonesha kuwa kuna walakini katika kushughulia suala hilo, na inadhihirisha kuwa ama wabunge au Spika wanataka kumtoa kafara Jairo!

Spika Makinda angefanya jambo la busara endapo angeipokea taarifa hiyo na kuisoma kwa wabunge ili kwa pamoja watambue ni upungufu gani uliomo, na si kukurupuka peke yake kudai kuwa ina walakini!

Ikumbukwe kuwa katika orodha ya fomu ya malipo kwa viongozi wa Bunge kuhusu semina ya wabunge ya sekta ya umeme nchini Juni 26, 2011 inaonesha jina la Spika Makinda akiwa miongoni mwa waliosaini kuchukua fedha zilizokusanywa na Jairo sh. 280,000, likiwamo pia ya Waziri Mkuu, Pinda.

Mpango uliosukwa

Lakini inaonesha kinachomtokea Jairo ni matokeo ya mpango uliosukwa tangu awali kwa lengo la kumuondoa madarakani kutokana na kuwaminyia ulaji baadhi ya viongozi wakiwemo wa kisiasa ambao walitaka kuitumia sekta ya nishati na madini kwa maslahi yao.

Mwanasheria nguli nchini, Dk. Masumbuko Lamwai aliwahi kukaririwa na Jambo Leo akisema kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatakiwa kuelewa kuwa kazi yake ni kutunga sheria na si kuongoza nchi, kwani dhamama ya uongozi wa nchi iko chini ya rais.

Dk. Lamwai alitoa kauli hiyo kuhusu utaratibu uliofanywa na Bunge katika kuchunguza tuhuma zinazomkabili Jairo.

Alisema yeye kama mwanasheria mwandamizi na aliyebobea, analoliona Bunge la Tanzania kutokuwa na uelewa wa kisheria, badala yake kufanya kazi ambazo kisheria ni kukiuka katiba ya nchi na taratibu za utawala bora.

Alisema Bunge lilikaa kama Mahakama ya Rufaa na kusikiliza kesi ya Jairo kisha kutoa hukumu kuwa ana hatia, mamlaka ambayo kikatiba na kisheria ni kuingilia mhimili wa Mahakama.

Bunge lilitumia ubabe

Niliwahi kueleza katika makala zangu siku za nyuma kwamba Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni, iliwasilisha taarifa yake huku ikiwakangaa Jairo na Luhanjo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Injinia Makani, aliliambia Bunge kuwa wengine wanaopaswa kuwajibishwa ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Naibu wake, Adam Malima na CAG, Utouh.

Fomu ya posho ya kujikimu inaonesha pia Waziri Ngeleja na Naibu wake, Malima kila mmoja alisaini kupokea sh. milioni 8 zilizokusanywa na Jairo.

Makani alisema baada ya kufanya uchunguzi wake uliowezesha kuwahoji watu 146, ilibainika kuwa utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kutoka katika taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kusaidia upitishaji wa bajeti bungeni, haukuwa wa kawaida na kwamba ulikiuka taratibu na sheria za fedha.

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha utaratibu huo wa wizara kukusanya fedha kwa taasisi zake ni mfumo uliokuwepo tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961, enzi za utawala wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Nasema hivyo kwa sababu ushahidi unaonesha kabla ya Jairo, Juni 19, 2009, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi aliwahi kuandika barua kama ya Jairo ya maombi ya fehda kwa taasisi ili kuwezesha uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya mwaka 2009/10 bungeni Dodoma.

"Fedha zilizokusanywa zilikuwa kwa matumizi ambayo yasingehitaji uchangishaji kwa sababu yangeweza kugharamiwa na kasma zilizopo za wizara.

"Uchangishaji huo ulisababisha taasisi hizo kubebeshwa mzigo kwa kuwa hazina kasma mahususi kwa ajili ya kuchangia wizara kwa ajili ya maandalizi ya uwasilishaji wa bajeti bungeni," alisema Makani.

Alisema utafiti ulibaini kwamba Jairo akiwa Katibu Mkuu, aliomba fedha kiasi cha sh. milioni 180 kutoka taasisi nne ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililoombwa sh. milioni 40, Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) sh. milioni 40, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) sh. milioni 50 na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) sh. milioni 50.

Hata hivyo, kiasi kilichochangwa ni sh. milioni 140 tu kutoka Tanesco, REA na TPDC wakati Ewura waligharamia chakula cha mchana wa siku tatu pamoja na tafrija iliyokuwa imepangwa kufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti ambayo iliwagharimu sh. milioni 9.7.

Makani aliongeza kuwa uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mbali na fedha hizo, kulikuwa na kiasi kingine cha sh. milioni 428.8 kilichotoka katika idara mbili za wizara hiyo ambazo ni Idara ya Uhasibu sh. milioni 150.7 na Idara ya Sera na Mipango iliyotoa sh. milioni 278 kwa ajili ya kusaidia upitishaji wa bajeti.

Alisema fedha zote hizo jumla yake ikiwa sh. milioni 568.8, ziliingizwa kwenye akaunti ya taasisi ya GST iliyopo mjini Dodoma, lakini akasema kati ya hizo, sh. milioni 150.7 zilikuwa kwa ajili ya gharama za vikao na semina na kiasi kilichokuwa mahususi kwa ajili ya uwasilishaji wa bajeti bungeni kilikuwa ni sh. milioni 418.8.

Makani alibainisha kuwa maelezo waliyopewa na wizara husika, walifikia uamuzi wa kuomba fedha hizo kutokana na fungu ambalo hutumika kwa ajili ya shughuli za bajeti kubakiwa na sh. milioni 35 tu kati ya sh. milioni 207 zilizokuwa zikihitajika.

Hata hivyo, alisema wizara haikuzingatia kanuni husika za fedha katika kuomba fedha hizo, na kwamba Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo alipohojiwa na kamati hiyo, alisema utaratibu uliotumiwa si halali.

"Sababu zilizoifanya Wizara kuchangisha fedha haziwezi kutiliwa maanani kwa sababu hadi kufikia Juni 25, 2011 Wizara ya Nishati na Madini ilikwishapata mahitaji yote ya fedha za uwasilishaji wa bajeti baada ya kupokea sh. milioni 171.5 za matumizi mengineyo (OC) kutoka hazina," alisema Makani.

Mkono alionya

Ndiyo maana wakati wa mjadala wa awali kuhusu Jairo, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM) alipinga uamuzi huo kwa kuliambia Bunge linakwenda nje ya mipaka kwa kuingilia taratibu za mihimili mingine kwa kumhukumu Jairo tena bila kumpa nafasi ya kujitetea!

Katika mgawanyo wa madaraka, Bunge linatakiwa kutambua kazi yake ni kutunga sheria, Mahakama ni kuzitafsiri na Utawala (Serikali) ina jukumu la kuzisimamia! Kwanini Bunge lisiheshimu utawala wa sheria? Kinachofanyika, Bunge linataka kujitwika mamlaka ya kuajiri na kufukuza watumishi serikalini, ndiyo maana wanatishia kwamba eti kama Jairo anarejeshwa kazini, basi Pinda ajiuzulu! Si sahihi.

Athari za Bunge kuingilia kazi zisizo zake tumezishuhudia mara kadhaa nchini. Wabunge walijifanya ni wataalamu wa masuala ya umeme, wakashinikiza mitambo isinunuliwe au uwekezaji usifanyike kwa ushauri wa Bunge, wakasema bora nchi iingie gizani kuliko kuwasha mitambo ya Dowans ambayo sasa imewashwa kwa gharama baada ya kutofanya kazi kwa miaka mitatu!

Wabunge hawana budi kuheshimu watalaamu na mihimili mingine na kila chombo kifanye kazi yake badala ya kutafuta umaarufu usio na manufaa kwa Taifa.

Kinachofanywa na wabunge ni kituko kwa mtazamo wangu... Iliundwa tume ambayo tayari ilikuwa na majibu. Katika kikao cha Bunge kilichofikia tamati juzi, wabunge walitumia ripoti ya CAG kuwabana mawaziri... hapo ripoti yake inaaminika. Kwa nini alipotoa ripoti ya Jairo hakuaminika? Mbona taarifa zake zote hazijawahi kukataliwa na Bunge? Kwa nini hii ya Jairo?

Kinachoonekana ni kwamba Jairo tayari alikuwa amehukumiwa na wabunge hata kabla ya kesi yake kusikilizwa kwa haki. Binafsi nakosa imani na Tume iliyoundwa na Bunge kwa sababu wao walikwishamhukumu mapema kabla ya kesi yake.

Kwa hili hapana!

Katika uchambuzi wangu siku zilizopita, hasa lilipoibuka sakata hili la Jairo, niliwahi kuandika kwamba: 'Wabunge mnataka mtuhumu, mchunguze, mwendeshe kesi, mtoe hukumu... hapana!

Narudia kusema kwamba, waliofuatilia vikao vya Bunge vilivyomalizika mjini Dodoma, hapana shaka watakubaliana nami kwamba Bunge sasa limegeuka kuwa uwanja wa kuwashambulia na kuwasulubu watu ama walio au wasiokuwa wabunge.

Ninachokiona ni kwamba sasa wabunge wanakigeuza chombo hicho kuwa cha kuwaonea na kuwakandamiza watu walio nje ya Bunge, badala ya kulinda na kutetea haki za watu, hususan wanyonge wasio na sauti.

Ingawa Katiba ya Tanzania inawapa kinga wabunge ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai au madai ya mambo wanayoyasema bungeni, kwa lengo la kulinda uhuru wa majadiliano ya Bunge, lakini kinga na uhuru huo haviwezi kuwa nyenzo ya kuwadhalilisha watu wengine.

Nashangazwa na hatua ya Bunge kuvuruga sheria za nchi na Katiba ambayo inampa haki zake za msingi  kila Mtanzania akiwemo Jairo.

Wabunge wamefikia hatua ya kujibinafisisha madaraka ambayo hawatakiwi kuwa nayo yakiwemo ya kuchunguza, kuendesha mashtaka na kuhukumu, kazi zinazotakiwa kufanywa na Polisi, Mahakama na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

Haiwezekani tuhuma ikaibuliwa bungeni na wabunge hao hao wakafanya kazi ya kuchunguza na baadaye kutoa hukumu. Kauli ya Spika Makinda inadhihirisha wabunge wanata Jairo 'anyongwe'.

Naamini wabunge wamekuwa wakitumia vibaya upendeleo huo wa kisheria, hali inayotia shaka kuhusu uhuru na kinga hiyo ya Bunge unaoonesha uonevu wa dhahiri kwa wanyonge.

Na sasa inaonesha dhambi hiyo ya kuwaonea walio nje ya Bunge, imeanza kuwageuka na sasa wanataka kutafunana wao kwa wao, ndiyo maana katika kikao cha Bunge kilichofikia tamati juzi, uliibuka msuguano uliotia shinikizo la kutaka baadhi ya mawaziri wajiuzulu kwa madai ya utendaji kazi wao usioridhisha.

Katibu wa Wabunge wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama aliwaambia waandishi wa habari kuwa walikubaliana kwamba kikao cha wabunge wa CCM kilifikia uamuzi wa kuwashinikiza mawaziri nane kujiuzulu, na kwamba ungetolewa na Mwenyekiti wa wabunge wa chama hicho ambaye ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Pinda alikaririwa awali akisema kuwa angezungumzia mustakabali wa mawaziri hao Jumatatu, kwa vile alikuwa hajapokea barua yoyote ya waziri aliyejiuzulu.

Mawaziri waliotajwa kushinikizwa kujiuzulu ni Waziri wa Uchukuzi, Nundu, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Mkuchika.

Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Cyril Chami na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe.

Lakini uchunguzi unaonesha kuwa sehemu kubwa ya tuhuma zinazotolewa kwa mawaziri hao kwa mujibu wa ripoti za kamati za kudumu za Bunge, ni kutokana na chuki binafsi, mgongano wa maslahi na vyeo.

Sasa wanageukana!

Kwa mfano, Waziri wa Uchukuzi, Nundu, alilazimika kumwaga 'mboga' baada ya baadhi ya wabunge kumtuhumu kwamba amefuja fedha za umma. Ni dhahiri kuwa baadhi ya ripoti zinazotolewa na kamati za Bunge zimejaa walakini na watu kukomoana!

Waziri Nundu aliamua kumtwisha mzigo Naibu Waziri wake, Dk. Athuman Mfutakamba, kuwa ndiye aliyeshinikiza Kampuni ya China Communication Construction (CCC) kujenga gati namba 13 na 14 baada ya kugharimiwa safari nje ya nchi bila idhini yake!

Lakini inavyoonesha, Waziri Nundu anataka kutolewa kafara katika hili kwa sababu ya msimamo wake kuhusu CCC kwamba wasipewe tenda ya kujenga gati hizo kwa sababu zingeigharimu Serikali.

Mbali na mvutano wa Nundu na Mfuatakamba, katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Biashara pia kumeibua mambo mazito yanayoonesha kuwa Waziri, Dk. Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu hawapikiki chungu kimoja.

Nyalandu alifichua waraka wake uliombebesha mzigo Dk. Chami katika sakata la kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege.

Waraka huo unaonesha kuwa Nyalandu alimshauri Dk. Chami amsimamishe kazi Ekelege kupisha uchunguzi wa CAG kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, lakini waziri hakuchukua hatua, hivyo kutafsiriwa kuwa alikuwa anamkingia kifua.

Waziri Chami alijitetea kuwa hakufanya hivyo kwa sababu Ekelege ni mteule wa rais, hivyo hakuwa na mamlaka ya kumsimamisha kazi; ingawa hakueleza kama alimshauri rais kuhusu hatua sahihi za kuchukua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu huyo wa TBS.

Si kwamba nawatetea mawaziri wanaotuhumiwa, lakini isionekane dhahiri kuwa wanaundiwa vikundi vya hujuma ili waumizwe bila makosa.

Nasema hivyo kwa sababu wabunge wanaonesha wanataka kuligeuza Bunge kuwa mahali pa kumalizia hasira zao binafsi dhidi ya watu waliowakosea ndani na nje ya Bunge, wanalitumia Bunge kuwakomoa mahasimu wao, kinyume cha malengo ya kuchaguliwa kwao.

Wabunge wanafedhehesha kwa vile wanaonesha matumizi mabaya ya kinga na uhuru waliopewa, wanadiriki kuwashambulia na kuwahukumu watu wengi tu walio nje ya Bunge.

Ikumbukwe kuwa si kila linalosemwa na mbunge bungeni ni la kweli, kuna mambo mengi ya uongo yanasemwa na wabunge wanapozungumza 'mjengoni', wakilenga ama kuwafurahisha wapiga kura wao au watu wengine wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi.

Tangu mwanzo wa suala la Jairo lilipoibuka bungeni, niliandika uchambuzi kwamba hana hatia kwa vile alitimiza wajibu wake, na ndicho CAG alichothibitisha, lakini nikashangaa wabunge wanamshupalia huku wakiungwa mkono na baadhi ya wana-habari.

Niliwahi kuandika kwamba inaonesha nchi hii itaangamizwa na watu wa aina mbili, wanasiasa na vyombo vya habari kwa sababu hakuna uchunguzi makini na upembuzi yakinifu, watu wanayugayuga (hangaika huku na huku) ilimradi siku zinapita.

Swali la kujiuliza, kama CAG aliyemchunguza Jairo alikuta hakuna makosa, wabunge wanadai kuna makosa, wanalazimisha kwa kutaka Jairo ashtakiwe, achukuliwe hatua, kwa kosa lipi? Kavunja sheria ipi?

Tukiendekeza haya mambo ya kila mtu akitoa tuhuma, fulani afukuzwe kazi tu kwa hisia, watafukuzwa wengi kwa kuonewa. Nimegundua nchi hii uzushi unatawala kuliko ukweli.

Jairo alisimamishwa na mkuu wake wa kazi, Luhanjo, na kwa niaba ya kupata ukweli akaamuru CAG afanye uchunguzi. Taarifa ya kumsimamisha na kumchunguza ilitolewa mbele ya waandishi, wabunge wanashupalia eti wapelekewe wao, kwani wao ndiyo walimtuma?

Uchunguzi ulipokamilika taarifa alipewa aliyekuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, baada ya kuipitia akaamua kuitoa au kutangaza matokeo kwa waandishi, wabunge wakahamaki na kutaka ripoti hiyo ipelekwe kwao wao ndiyo waijadili, ina maana wao ndiyo waliamuru Jairo achunguzwe?

Ndiyo maana hata ripoti ya Kamati Teule ilimkandamiza, kwa vile tayari walikwishamhukumu, na waliounda kamati wasingeweza kwenda kinyume cha matakwa ya wabunge, lazima wangewalinda wenzao kama walivyofanya! Ndivyo anavyotaka kufanya Spika Makinda.

Wabunge wanadhani wao ni 'superior', wanatuhumu, wanataka wachunguze, waendeshe kesi na watoe hukumu, wanataka wawe mawakili wa utawala wa sheria na kanuni ... hii ni hatari.

Bunge letu linataka kuwa Mahakama. Kwa hili la Jairo (anayetafutwa zaidi), Bunge linavunja utaratibu wa kikatiba.Awali, Bunge lilitoa hukumu hata kabla ya kuundwa kwa Kamati Teule ya uchunguzi. Serikali ilitekeleza utaratibu wake, wabunge wakalalamika kwamba Bunge limedharauliwa! Kwanini walitaka Jairo akutane na wabunge ilhali yeye si mwanasiasia kama wao?

Ndiyo maana nasema Bunge linafanya ubabe, hasa ukirejea nukuu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba: "Kama ni dharau zenu fanyeni huko huko, si hapa bungeni'! Hiyo tayari ni hukumu tosha.

Uonevu kwa Jairo ni kumtuhumu na kumhukumu, wakati mamlaka yake ya nidhamu ilimuondolea tuhuma zilizotolewa awali. Pia wakati wa mjadala husika, alionekana kwamba anapaswa kuondolewa kazini... tayari hapo ni hukumu bila hata uchunguzi.

Wabunge watambue kwamba wanatakiwa kushauri na kusimamia utendaji mzuri wa kufuata sheria na kanuni na si jazba na chuki! Walichokifanya wabunge wanataka kujihakikishia jinsi ya kurudi 'mjengoni' mwaka 2015. Hii ni vita ya ubinafsi. 

Willy Edward ni Mhariri Mkuu Jambo Leo. 0786-294384 /0655-294384 / 0763-394384.

Ciao...
Chanzo: Kamanda wa Matukio Blog