Tangazo

May 31, 2012

DROO YA TANO YA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, YANGURUMA TENA, MWANZA WAENDELEA KUVUNA ZAWADI

Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Jenereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam. Katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na (kulia) ni Abdallah Hemed kutoka Bodi ya Mchezo ya Kubahatisha.
*********************

Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi waliojitokeza kushiriki na kushinda zawadi zinazotolewa katika promosheni ya kipekee ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti limeendelea wiki iliyopita katika mikoa ya Iringa na  Mwanza ambapo mshindi wa jenereta na yule wa bajaj walikabidhiwa zawadi zao katika sherehe zilizohudhuriwa na umati mkubwa wa watu na kushuhudia SBL ikikabidhi zawadi hizo na kuamsha hamasa kubwa kwa wapenzi na watumiaji wa biadhaa za SBL.

Asubuhi ya leo droo ya tano ya promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya tano ya promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo bw. Ephraim Mafuru, amesema “Tumeshakabidhi jereta nne kwa washindi mbalimbali na zawadi ya pikipiki, bajaj mbili na gari moja aina ya FORD FIGO ambapo zawadi zote zimeshakabidhiwa kwa washindi wetu .  Hivi karibuni tutasafiri  kwenda Mafinga Mkoani Iringa kukabidhi Bajaj”.

“Naendelea kuwashauri jamii na watanzania kwa ujumla kwamba promosheni hii ni kwa ajili ya kila mtanzania mwenye vigezo vya kushiriki kwa hiyo wajitokeze k kwa wingi kushiriki ili kujaribu bahati kama wenzetu ambao wamejaribu na kupata zawadi kubwa ambazo hawakutarajia katika maisha yao.” Alisema  Mafuru.

Aliongeza kuwa zawadi zinazoshindaniwa gharama yake ni jumla fedha za kitanzania milioni 780 ikiwemo pesa taslimu ambazo mshindi anapata papo hapo kupitia matandao wa simu za mikononi M- pesa. Ikumbukwe kuwa zawadi hizi zinapelekwa hadi pale mshindi wetu alipo bila yeye kuchangia chochote walakugharamia chochote ikiwemo usafiri.

Katika droo hii ya tano mshindi ni Isaya Charles kutoka Igoma mkoani Mwanza ambaye amejishindia Jenereta, wakati mshindi mwingine Mariam Karumba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Saint Agustin pia anatoka mkoani Mwanza amejishindia Bajaj

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bidhaa yake bora kabisa ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager and Pilsner inaendesha promosheni hii kwa wiki 16 ikiwa na lengo la kuinua na kuboresha maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Safari Lager yatangaza Zawadi kwa Wajasiriamali Washindi wa “WEZESHWA NA SAFARI LAGER"

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika programu ya ruzuku ya“Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam leo.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
**************Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali.

Shelukindo alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. 

Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”

Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hao, Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. 

Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. 

Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea.

Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano" alisema.

Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. 

Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi na Damas Daniel Msoka.

Wengine ni pamoja na Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi.

Aidha aliwataja washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.

 Kituo cha Mwanza ni pamoja na Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. 

Katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwaluaja na Tatu Ngemela.

TIP OF THE DAY


RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BENKI YA MAENDELEO AFRIKA - afDB


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 2012.




Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana Mh Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dkt Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco Bw Omar Kabbaj (kushoto) , Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (wa pili kuhsoto) muda mfupi kabla ya kuzindua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Afruka katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31, 2012.PICHA/UKULU

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL NA MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA IRAN WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA PAMOJA KATI YA IRAN NA TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakisaini mkataba wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012. Picha na Amour Nassor-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakibadilishana mkataba baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012. Picha na Amour Nassor-OMR

NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Mkurugenzi Wa Masoko wa Benki ya NMB, Imani Kajura akifafanua jambo juu ya Promosheni mpya ya Jenga Maisha yako na NMB wakati wa uzinduzi wake Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Masoko wa NMB, Shilla Hatibu Senkoro.

Imani Kajura akionesha moja ya vipeperushi vya Promotion hiyo mpya ya NMB kwa wateja wake.
********
NMB ikiwa ni benki yenye kujali malengo ya wateja wake, inaanzisha promosheni inayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda; tani ya saruji, mabati ya kuwezekea, amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB au mabegi ya shule kupitia promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB. Promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB itachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu.

NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea na pia kuboresha maisha yao.

Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye za NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.

Baada ya ubinafsishaji wa benki ya NMB mwaka 2005, NMB iliendelea kukuza mtandao wake wa matawi, ndani ya miaka mitano matawi yameongezeka kutoka 100 hadi matawi zaidi ya 140. Idadi ya wateja wa NMB imekua kutoka wateja 600,000 mpaka wateja 1,600,000 hiyo ni asilimia 30 au 40 ya watanzania wote ambao wana akaunti katika benki zote za Tanzania ili kurahisisha na kuboresha utoaji huduma.

NMB ilianza kutoa huduma ya ATM kutoka wateja 0 mpaka wateja milioni moja na laki sita na pia namba za mashine za kutolea fedha (ATM) zimekuwa kutoka 0 mpaka 450 na pia NMB ndio benki ya kwanza Tanzania kuanzisha huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi, NMB Mobile. Hadi sasa kuna wateja 600,000 wanaotumia huduma ya NMB Mobile

NMB imeendelea kubuni na kuanzisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wateja wake. NMB ndio benki pekee Tanzania yenye akaunti kuanzia za watoto wadogo, wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wastaafu. Pia NMB imeendelea kuboresha faida wateja wanazozipata kutokana na kuwa na akaunti NMB.

Hivisasa mteja wa NMB ana chaguo pana la njia za kupata huduma; anaweza kupata huduma ndani ya benki, kutumia ATM, kutumia NMB mobile au huduma ya Intaneti.

NMB ni benki inayowajali sana wateja wake hata wakati wa shida, mwaka jana, 2011 NMB ilizindua huduma ya NMB Faraja inayomwezesha mteja wa NMB Personal Account kupata mkono wa pole kati ya shilingi 600,000 hadi 1,200,000. Hadi sasa, huduma ya NMB Faraja imewanufaisha wateja wengi wa NMB, nchi nzima.

Utafiti uliofanywa na NMB uligundua kuwa wateja wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea. Miongoni mwa malengo hayo ni kujenga nyumba, kusomesha watoto na kufikia malengo mengine muhimu maishani mwao.

VIDEO: JESTINA GEORGE ON AFRICAN FASHION & DESIGNS

Jestina George is a fashionista, blogger, Presenter and a model based in London, from Tanzania the land of Kilimanjaro. AILTV caught up with her at the the launch of READY TO WARE by Anna Luks. Jestina is speaking is expressing her concerns about African fashion and designs.

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAFUNZO YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana Mei 30, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana Mei 30, 2012 mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye lpia ni Mwenyekiti wa Tume ya  Mabadiliko ya Katiba ambaye alizungumza katika Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha  Saint Gaspar Mjini Dodoma Mei 30,2012. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Bilal akiteta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kufunga mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar Mjini Dodoma Mei 30, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wabunge wa Chadema waagwa rasmi kwa kuangalia mechi ya kimataifa kati ya US na Brazil.

Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la Chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter  Msigwa na  Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011  waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini Marekani. PICHANI: Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.

Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa. 

Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini Marekani.

Na bendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar.

Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.(Picha & maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

Katuni ya Leo


KILIMANJARO TAIFA STARS WAONDOKA ALFAJIRI YA LEO KUELEKEA ABIDJAN



Wachezaji wa Kilimanjaro Taifa Stars wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana (Alhamisi asubuhi) kuelekea Abidjan kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Ivory Coast ya kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumamosi. 
********************
 
Kikosi cha wachezaji 23 na viongozi tisa imeondoka leo 31 Mei, 2012 saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 2 mwaka huu.

Wachezaji wanaoondoka ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Nassor Masoud Cholo, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.

 Wengine ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva, Haruna Moshi na John Bocco.

 Wachezaji waliobaki kutokana na kuwa majeruhi ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari.

 Viongozi waliofuatana na timu hiyo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Msafara huo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori wakati naibu kiongozi wa msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir Haji.

Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeagwa jana (Mei 30 mwaka huu) na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vizuri Tanzania kwenye mechi hiyo.

 Hafla hiyo ya kukabidhi Bendera ya Taifa pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.

 Mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.

 Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.

 Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.

 Stars itarajea nyumbani Juni 5 mwaka huu saa 1.40 na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

May 30, 2012

Airtel yaongeza Zawadi ya Milioni 143/- katika Promosheni ya 'Nani Mkali'


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akitangaza  kuongezeka kwa  zawadi ya  hadi Milioni 143 /- katika Promosheni ya Nani Mkali itakayoendelea kwa muda wa Miezi Miwili zaidi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 30.12. Ili kushiriki promosheni hiyo andika  neno “Mkali” tuma kwenda  15656 bure. Baada ya hapo Mteja atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa 350/- pamoja na kodi. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi. Dangio Kaniki.

Polisi Ruvuma yawashikilia Watu wawili kwa tuhuma ya Mauaji ya Mtoto

Mama wa Mtoto, Jema Msemwa (19)
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limewatia mbaroni watu wawili wakazi wa eneo la Mkuzo katika halmashauri ya manispaa ya Songea ambao wana uhusiahano wa kimapenzi kwa tuhuma za kumuua mtoto mdogo wa jinsia ya kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu  kwa madai kuwa mtoto huyo amekuwa akikwakosesha starehe zao za kimapenzi pale wanapohitaji kukutana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa mbili na nusu asubuhi huko katika eneo la Mkuzo ambako inadaiwa kuwa mtoto huyo aliuwawa kwa kunyongwa shingo na watuhumiwa ambao aliwataja kuwa ni Jema Msemwa (19) na Yohana Njelekela (22) wote wakazi wa Mkuzo.

Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa Mei 29 mwaka huu majira ya saa za asubuhi huko katika kituo cha polisi cha mjini Songea ilipokelewa taarifa kuwa kuna binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Jema mkazi wa Mkuzo ambaye alikuwa na mtoto mdogo wa kike aitwae Rebeca Cheni (1.3) alikuwa amefika nyumbani kwa dada yake akiwa hana mtoto jambo ambalo lilipelekea kuanza kuwa na mashaka naye.
Mwili wa Mtoto ukiwa Mortuary
Alisema kuwa Jema baada ya kuulizwa na dada yake kuhusu mtoto ndipo alijibu kuwa amemuacha kwa mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Hamisi ambaye alidai kuwa anaishi eneo la Luwawasi, hivyo kwa kushirikiana na mume wa huyo dada yake walimlazimisha Jema waende kwa Hamis  kumchukua mtoto.

Lakini wakiwa njiani kabla hawajafika Jema alibadili maelezo yake na kusema  kuwa hajui alikomuacha mtoto wake ndipo dada yake alipoamua kumfikisha katika kituo cha polisi ili waweze kupata msaada zaidi wa kubaini mahali alikomuacha mtoto.

Alibainisha zaidi kuwa Jema alipofikishwa katika kituo cha polisi alihojiwa kwa kina zaidi ndipo alipoeleza kuwa mei 27 mwaka huu akiwa ametokea Njombe huku akiwa na mtoto wake na siku iliyofuata majira ya saa saba mchana aliondoka nyumbani kwa dada yake na kuelekea kwa mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Hamisi ambako alidai kuwa anaenda kulala.

Alieleza zaidi kuwa Jema baada ya kufika huko walishauriana na mpenzi wake watoke kwa matembezi na ilipofika majira ya saa moja usiku walirudi nyumbani kwa Hamisi ndipo Jema aliulizwa na mpenzi wake Hamisi kuwa mtoto huyo hatembei wakati ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu, na Jema alimjibu kuwa hata yeye mpaka sasa jambo hilo linamsikitisha.

Kamanda Kamhanda alisema kuwa baada ya maelezo hayo inadaiwa kuwa Hamisi alikasirika na hatimaye alimweleza Jema kwakuwa mtoto huyo si wa kumzaa yeye lazima amuue ili amuoe Jema ili waendelee kuishi vizuri zaidi jambo ambalo Jema hakukubaliana nalo na alitoka nje ya nyumba na kumwacha mtoto akiwa amelala kitandani kwenye chumba cha Hamisi.

Alisema Jema aliporudi ndani ya chumba hicho alimkuta mtoto wake akiwa anakoroma na baada ya kumuuliza Hamisi kulikoni alimjibu kwa ukali na kumtaka ambebe mtoto wake aondoke, hivyo Jema akamchukua mtoto wake na kuelekea nyumbani kwa dada yake na kabla hajafika nyumbani kwa dada yake Hamisi alimfuata kwa kutumia pikipiki na kumsihi Jema asiende kwa dada yake na badala yake mtoto huyo wakamtupe lakini pia wakiwa njiani majira ya saa nne usiku Jema aligundua kuwa tayari mtoto huyo alikuwa amekwisha fariki Dunia ndipo wote kwa pamoja walielekea eneo la Bombambili mtoni ambako walimficha mtoto huyo kwenye kichaka kwa kumfunika kitenge. Na baada ya tukio hilo Jema na Hamisi walirudi nyumbani kwa Hamisi.

Kamanda Kamhanda alisema kuwa mei 29 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi, Jema aliondoka nyumbani kwa Hamisi na kuelekea nyumbani kwa dada yake akiwa hana mtoto na alipofika dada yake alimuuliza mtoto yuko wapi na alijibu kuwa mtoto yupo kwa Hamisi jambo ambalo halikuwa la kweli ndipo dada dada yake alifikisha taarifa katika kituo cha polisi ambapo askari walimhoji Jema na alikiri kuwa mtoto wake Rebeca amefariki na alikwenda kuwaonyesha mahali ambapo mwili wa marehemu ulikuwa umefichwa.

Alisema kuwa kwa uchunguzi wa polisi wa awali unaonyesha kuwa mwili wa marehemu Rebeca haukuwa na jeraha lakini shingo yake ilikuwa imelegea na ilionekana kuwa alifariki kutokana na kunyongwa shingo na upelelezi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa aliyejiita Hamisi baada ya kukamatwa mei 30 mwaka huu majira ya saa tisa usiku akiwa amelala nyumbani kwake alifahamika kuwa jina lake halisi ni Yohana Njelekela na siyo Hamisi kama alivyokuwa akimdanganya Jema.

Hata hivyo Kamhanda alisema kuwa polisi inaendelea kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo na kwamba utakapokamilika watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalowakabiri.
Habari kwa hisani ya Songeayetu Blog

Rais Kikwete ateua Wakurugenzi Wapya Tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteua Wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo, Jumatano, Mei 30, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu, 2012.

Walioteuliwa ni Ndugu Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Ndugu Naimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; Ndugu Celestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; Ndugu Yahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na Ndugu Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.
 
Wengine ni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; Ndugu Dorah Msechu ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika, Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, na Ndugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi wake,  Ndugu Kibwana  alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu Naimi Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, na Ndugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

Naye Ndugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.    
                                ..……..Mwisho……….

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2012


TAIFA STARS KWENDA ABDIJAN KESHO

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla akimkabidhi bendera ya taifa Nahodha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Juma Kaseja wakati wa kuiaga timu hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Kwa Hisani ya Habari Mseto Blog).

Charles Taylor aenda Jela Miaka 50

Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.

Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.

Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.

Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.

Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi.

Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kutumikia kifungo chake nchini Uingereza.

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo Mei 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.PICHA NA IKULU

Wakiwa katika picha ya pamoja.

Uongozi wa Chadema wakutana na Balozi Maajar - Washington DC

Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja  na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter  Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc.

Wabunge wa Chadema  Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi  Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi  Mhe.  Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.

Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATEMBELEA MRADI WA NYUKI WA PINDA - DODOMA


Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakitembelea mradi wa ufugaji nyuki katika Shamba la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo eneo la Zuzu Dodoma Mei 29,2012. Viongozi hao wako Dodoma kwa semina. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu kifaa maalum kinachotumika kukamuwa asali kutoka kwenye masega wakati Wakuu wa Mikoa na Wilya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa walipotembelea mradi wake wa ufugaji nyuki,eneola Zuzu Dodoma, Mei 29,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

"Hongera Bi. Christina Rweyemamu kwa kupata Mapacha Watatu"

Mkazi wa jiji Christina Rweyemamu akiwa mwenye tabasamu huku akiwa na watoto wake mapacha watatu wote wa kike (kutoka kushoto), Nyangoma, Nyakato na Nyamwiza, aliojifungua Mei 05.2012, katika Hospitali ya Dk. Kairuki kama alivyonaswa na kamera yetu nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  PICHA ZOTE/DENNIS ISHENGOMA
 

"Mapacha watatu, Nyangoma, Nyakato na Nyamwiza, wakiwa wametulia.

JK ampokea Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast jijini Arusha


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Allasane Ouattara uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Kilimanjaro jijini Arusha Mei 29.2012, akiwa ni mmoja wa wageni mashuhuri kuhudhuria mkutano wa afDB. Picha na IKULU

May 29, 2012

Hatimaye Mtuhumiwa John Warburg atiwa nguvuni na Polisi baaya ya Kuruka Dhamana Kituo Cha Urafiki




Kachero kutoka Polisi Arusha, D/CPL Fortunatus (mwenye tisheti ya pundamilia kushoto), akiimarisha ulinzi wakati Mtuhumiwa wa Kesi ya Wizi wa Kuaminiwa, Bw. John Warburg (mwenye tisheti nyekundu), akiteremka kutoka kwenye Bus la Ngorika katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam leo Mei 29.2012, wakitokea jijini Arusha ambako Mtuhumiwa Warburg alikamatwa kufuatia kuruka dhamana aliyopatiwa katika Kituo cha Polisi cha Urafiki takribani Miezi Mitatu iliyopita. John Warburg alidhaminiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa kosa la kujipatia Gari aina ya Toyota Cresta GX 100 lenye namba za usajili T 796 AVQ na kuliuza kwa manufaa yake bila idhini ya mwenye mali kesi yenye kumbukumbu namba URP/RB/2412/2012 -.URP/IR/1544/2012. PICHA/DAILY MITIKASI BLOG

Mdhamini wa Mtuhumiwa John Warburg bwana Max Kafipa (kulia), akiwa bega kwa bega na mtuhumiwa wake kuhakikisha anafika Kituo cha Polisi Urafiki.Kushoto ni D/CPL Fortunatus wa Polisi Arusha, aliyemu-escort mtuhumiwa hadi hapa jijini.